Rafiki yangu mpendwa naamini upo kama unapenda kuwa chanya mara zote kwa kufanya yale yanayochangia uchanya kwenye maisha yako.
Ili uweze kusema hapana kwenye mambo yasiyo sahihi kwenye maisha yako, lazima uwe una mambo sahihi unayosema ndiyo.
Lazima ndiyo yako iwe kubwa na muhimu kuliko hapana. Sema ndiyo kwenye mchakato unaofanyia kazi na sema hapana kwa mengine yote ambayo hayasaidii mchakato huo.
Ndio, hapana zako zitawaumiza watu kwa muda mfupi, lakini zitawasaidia kwa muda mrefu kupitia kile unachofanya, ambapo kwa kusema hapana kwenye mengine utakifanya kwa ubora sana.
Lazima pia uwe na kiasi kwenye hapana zako, maana iwapo utasema hapana kwa kila kitu, itakuwa ni njia nyingine ya kujificha au unaweza kuwapoteza wale muhimu unaowahitaji sana kwenye kile unachofanya.
Ukisema ndiyo kwenye mambo mengi nako unakosa muda na umakini wa kutosha kwenye kile muhimu unachofanya.
Chukua hatua, rafiki yangu weka vipaumbele vyako kwa usahihi, sema ndiyo kwa yanayohusiana na vipaumbele vyako na hapana kwa yasiyohusiana.
Habari njema ni kwamba usiogope kuwaumiza watu kwa muda mfupi kwa hapana zako, kwani baadaye watanufaika na matokeo utakayozalisha.
Mwandishi wako,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.