Sheria Za Kuwa Na Maisha Marefu.

Rafiki yangu mpendwa leo tutachunguza kwa kina sheria za kuwa na maisha marefu na ya mafanikio bilionea na mwekezaji Charlie’s Munger ambaye kwa sasa ana miaka 99.

Aliulizwa na mwandishi aseme siri za kuwa na maisha marefu na ya mafanikio.

Moja ni usiwe na wivu. Wivu ni hali ya kujiona wewe una stahili kuliko mwingine.Ukiishi maisha ya wivu, hutaweza kufurahia maisha yako.

Waache watu waishi vile wanavyotaka wao na wewe ishi vile unavyotaka wewe.Usiwe na wivu na mtu.

Mbili ni usiwe na chuki. Watu wamekuwa na chuki za kijinga, hawapendi kuona wengine wamewazidi, wanakuwa na chuki ambazo hazina hata maana kwenye maisha yao.

Chuki ni mzigo mzito, usikubali kuubeba, kila siku kuwa mtu wa kusamehe na kuwachukulia watu kama walivyo bila kubeba matatizo yao binafsi.

Tatu ni usitumie zaidi ya kipato chako. Hapa kwenye fedha mchakato ni ule ule, haijalishi unaingiza kipato kikubwa kiasi gani, unatakiwa kutumia chini ya kipato chako.

Usiende juu ya kile unachopata. Na ukizingatia misingi hii, lazima utafika mbali.

Nne ni shauku. Shauku ndiyo sifa namba moja inayolipa zaidi duniani. Ukitaka kukubalika kila eneo la maisha yako basi ongea kwa shauku kubwa. Kila kitu unachofanya, kifanye kwa shauku kubwa.

Ukikutana na watu usiwe kama mtu ambaye hana shauku, ukikosa shauku kubwa kwenye maisha yako, hata kama una kitu kizuri ndani yako watu watakupuuza mara moja.Kuwa na shauku kubwa kwenye kila eneo la maisha yako.

Tano ni jihusishe na watu wanaoaminika. Kama una watu ambao hawaaminiki kwenye maisha yako achana nao kabisa. Anza kujihusisha na watu wanaoaminika na itakusaidia kupiga hatua kubwa kwenye maisha yako. Ukiaminika kwenye maisha yako, watu wengi watakuwa tayari kufanya kazi na wewe.

Sita ni fanya unachopaswa kufanya. Jua wajibu wako ni nini kisha kuwa tayari kufanya wajibu wako bila kukumbushwa. Watu wengi hawafanyi kile wanachopaswa kufanya, hivyo wewe ukiwa ni mtu wa kufanya kile unachopaswa kufanya bila kuambiwa utafanikiwa sana kwenye maisha yako.

Hatua ya kuchukua leo; ishi sheria hizi sita kwenye maisha yako, na jikumbushe kila siku pale unapoamka na kabla hujaenda kulala.

Sina uhakika kama itakufaa lakini ushauri wa Bilionea Charlie Munger unafanya kazi, kama yeye ni Bilionea na ni Mzee wa miaka 99 ameweza kuishi misingi hii basi na wewe ukiishi bila shaka na wewe utatoboa miaka kama yake au hata na zaidi.

Mwandishi wako,

Maureen Kemei.

kemeimaureen7@gmail.com.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *