Rafiki yangu mpendwa leo tunachunguza vitu vitatu vinavyosababisha shida kwenye maisha yetu.
Mfanyabiashara, mwekezaji na mwandishi Kevin O’Leary anasema kwenye maisha kuna wanaume, wanawake na fedha.
Mwandishi anasema, shida yoyote kwenye maisha, inatokana na vitu hivyo vitatu. Kama husumbuliwi na mwanamke, basi mwanaume anakusumbua. Na kama kwa mwanamke na mwanaume uko vizuri basi fedha itakua inakusumbua.
Kila mmoja wetu ana shida kwenye mahusiano yake au fedha, kama husumbuliwi na fedha basi unasumbuliwa kwenye mahusiano.
Na hakuna mtu ambaye amefanikiwa kupatia maisha kwenye kila eneo la maisha yake. Sina uhakika kama itakufaa lakini mwandishi anasema, sehemu kubwa ya matatizo ya wengi, inatokana na ukosefu wa fedha au tabia mbaya kwenye fedha.
Kwenye fedha kama una fedha basi utakua una tabia mbaya za fedha yaani kwenye kudhibiti fedha na matumizi kiujumla unapigwa chenga. Ila matatizo mengi tuliyonayo, yanatatuliwa na FEDHA tu.Ukiwa na fedha shida nyingi unazimaliza.
Leo nataka nikuulize swali, kama tatizo lako ukiwa na hela linaisha? Kama jibu ni ndiyo, basi huna tatizo. Kaa chini na ona njia zipi unaweza kutumia kupata fedha unazozihitaji ili kutatua tatizo hilo. Kama fedha inaweza kutatua tatizo linalokusumbua, basi tafuta fedha tu na tatizo lako litaisha. Kama tatizo lako halitatuliwi na fedha, basi iachie asili, muda ifanye kazi yake usijisumbue kwa matatizo ambayo hayatatuliwi na fedha.
Kama ni mwanaume au mwanamwake anakusumbua angalia njia ambayo mnaweza kuweka mambo yenu sawa. Kama inashindikana tafuta mwache asili itakusaidia kupambana naye wewe ishi maisha yako.
Hatua ya kuchukua leo; kama fedha inatatua tatizo lako, basi tafuta fedha achana na yale ambayo hayana msingi kwako.
Kumbuka, kwenye maisha kuna wanawake, wanaume na fedha, kipi ambacho kinafanya maisha yako yaweze kwenda? Mwanamke au mwanaume au fedha?
Kitu kimoja zaidi, fedha ndiyo jawabu la mambo yote, ukiwa na fedha utapata kile unachotaka kwenye maisha yako.
Mwandishi wako,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.