Umuhimu Wa Kuanza Na Wewe Kwanza.

Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini unapaswa kuanza na wewe kwanza, kama kuna watu hawakupi kile ambacho wewe unataka kwenye maisha yako, anza kwanza wewe mwenyewe kujipa kitu hicho ambacho unataka kutoka kwao.

Kwa mfano, kama unataka upendo kutoka kwa wengine, anza kwanza kujipenda wewe mwenyewe, penda kile unachofanya na kisha wapende wengine na utashangaa vile unavyotaka vitakuja vyenyewe.

Kama watu hawakuamini, huna haja ya kuwalazimisha wakuamini, unachotakiwa kufanya ni kuanza kujiamini wewe mwenyewe kisha wale ambao watakuamini watakuamini bila shaka yoyote ile.

Kama unawapa watu kazi na hawafuatilii maagizo unayowapa, anza wewe kuwafuatilia kwa karibu kwa kudai matokeo unayoyataka na wao watajituma kukamilisha hilo kwa sababu wanajua wasipofanya hawana ripoti ya kutoa.

Kama kuna watu umewakosea, unawaomba msamaha na hawataki, achana nao, jisamehe wewe mwenyewe ila maisha yako yaende.

Kama kuna watu hawakuheshimu, anza kujiheshimu wewe mwenyewe kwanza. Kama kuna watu  kwenye biashara yako wanakuambia haiwezekani waoneshe kwa mfano jinsi inavyowezekana kufanyika.

Kile ambacho sisi tunataka kitokee kwetu, tuanze  kwanza sisi kukiishi kwa kukifanyia kazi. Watu wakikuambia, huwezi kufanikiwa kwenye lengo lako, waambie inawezekana kwa vitendo. Kuwa bora wewe ili uweze kuwadhihirishia wengine kwamba mambo yanawezekana kama ukiyafanyia kazi.

Hatua ya kuchukua leo; kuwa mfano wewe mwenyewe wa kuishi kile ambacho wengine unataka wakufanyie.

Kanuni ya dhahabu inasema, watendee wengine kile ambacho wewe ungependa kutendewa. Nenda kalifanyie kazi hili na utakuja kunishukuru baadaye.

Mwandishi wako,

Maureen Kemei.

kemeimaureen7@gmail.com.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *