Kitu Kinachopoteza Zaidi Kwenye Maisha.

Rafiki yangu mpendwa, kinachokupoteza ni kujilinganisha na watu wa nje.
Unataka kuishi kama mtu ambaye tayari ameyapatia maisha, unataka kuishi kama mtu ambaye yuko katika nchi zilizoendelea na wakati wewe uko katika nchi zinazoendelea.

Kwa mfano, kwenye kazi unataka kufanya kidogo huku ukiwa na matarajio ya mfano makubwa. Unajilinganisha na mabilionea ambao wakati wanaanza walikuwa hawaishi maisha ya anasa, walikuwa wanafanya kazi usiku na mchana halafu wewe hujafikia viwango hivyo unataka kuishi kama wao.

Rafiki yangu, maisha ya nchi zinazoendelea ukizaliwa tu tayari umeshafungwa tatu bila , unapambana kwanza uweze usawazishe ndiyo uweze kushinda.

Maisha ya nchi zinazoendelea ni kama kupanda mlima, hivyo linapokuja suala la kazi wewe fanya tu kazi hata muda mrefu. Usiwasikilize watu wanaokuambia kwamba fanya kazi kidogo tumia akili.

Kila kazi inahitaji kazi, weka juhudi kubwa, mpaka sasa bado umefungwa tatu bila pambana usawazishe.

Ukizaliwa nchi zilizoendelea tayari umeshinda tatu bila unaona hapo utofauti?

Kitu kikubwa ambacho kinafanya watu wengi wa nchi zinazoendelea kutokupiga hatua ni kuishi kama vile nchi zilizoendelea.

Bado huna anasa ya kuishi maisha hayo, bado hujakuwa huru kiasi hicho.

Kuwa huru ni gharama, tafuta uhuru wako kwa kujitesa sasa hivi, acha usingizi, acha anasaa zote na weka kujuhudi kubwa kwenye kufanya kazi.

Hatua ya kuchukua leo; kwenye maisha kuwa mtumwa wa kitu fulani ambacho unajua ukikomaa nacho kitakupa uhuru.

Kumbuka, ili uwe huru lazima uchague kuwa mtumwa wa kitu fulani. Unachagua nini? Usiishi maisha ya kuigiza pambana usawazishe magoli matatu ambayo tayari umefungwa.
Kama maisha yako bado, uko kwenye umasikini, unapambana kusawazisha hutakiwi kuwa na anasa, unatakiwa kuweka kazi. Na hata ukiifia kazini ni ushujaa, punguza kuridhika wakati maisha bado yanakupiga.

Mwandishi wako,

Maureen Kemei.

kemeimaureen7@gmail.com.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *