Rafiki yangu nikupendaye, hofu ni zao la akili. Ni vitu ambavyo hata havipo, ni vitu ambavyo vinazalishwa ndani ya akili yako.
Pata picha mtu yuko mwezi wa tisa leo, anaanza kufikiria hivi mwezi wa kumi utakuwaje? Rafiki yangu, hata kwa wale wanaosali, Yesu aliwafundisha wanafunzi wake sala na kwenye sala hiyo hakuna mahali alipoomba mambo ya kesho ila leo tu. Tunayasumbukia yajayo na tunayaacha ya sasa. Utupe leo, mkate wetu wa kila siku, na hajasema kesho, ila leo.
Usihofie mambo kutokea, wewe siyo mdhibiti wa mambo kutokea au kiranja wa dunia wa kutaka dunia iende kama wewe unavyotaka iende.
Acha mambo yatokee kama yalivyopangwa kutokea, usiwe na wasiwasi na kitu chochote kile, asili inakulinda na kukutetea, wewe timiza wajibu wako tu.
Hatua ya kuchukua leo; usihofie kitu chochote kile, nenda kachukue hatua kubwa leo bila hofu, bila sababu yoyote ile.
Unachohofia hata hakipo, ni zao la fikra yako, usijifunge na hofu jifungue kwa kuchukua hatua na utaona mambo yanaenda.
Mwandishi wako,
Maureen Kemei.