Mambo 5 Yanayosababisha Changamoto Kubwa Kwenye Zama Hizi.

Rafiki yangu mpendwa jamii ya Kisasa zina maendeleo makubwa sana ukilinganisha na za asili.

Lakini zina changamoto makubwa ukilinganisha na za asili kama upweke ni mkubwa, magonjwa ya akili yapo kwa kiwango kikubwa na pia hali ya watu kujiua, ipo zaidi.

Changamoto hizi zinasababishwa na haya:

Moja; hali ya ubinafsi mkubwa, watu huweza kujitegemea kwa kila kitu, haoni umuhimu wa kushirikiana na wengine, hilo linafanya mtu awe pweke licha ya kuwa na kila kitu.

Pili; wingi wa watu, unafanya watu wasijuane kwa undani. Watu wanaweza kuwa wanakata eneo moja lakini hawajuani, kila mtu anakuwa na maisha yake, linafanya jamii kukosa ushirikiano.

Tatu; kukosekana kwa usawa baina ya watu kwenye jamii. Wachache wana mali sana huku wengine wakiwa hawana. Linafanya ushirikiano baina ya wanajamii ukosekane.

Nne; ubadhilifu, kuwa watu ni wengi na hakuna ile hali ya kujuana moja kwa moja, baadhi ya watu wanaweza fanya ubadhilifu na wasijulikane. Ni vigumu kuwatambua na kuwajibisha.

Tano; kutegemea zaidi mamlaka ambazo haziwezi kutafuta kila kitu kwenye jamii. Kukosekana kwa ushirikiano wa karibu wa wanajamii kunapelekea wategemee mamlaka za kiserikali ambazo sinasimamia sheria na taratibu mbalimbali.

Lakini haziwezi kufika mpaka ngazi za chini kabisa, kama ambavyo watu wangeweza kuwajibishana wenyewe kwa wenyewe pale wanapojuana kiundani.

Sababu hizi zinawasukuma watu kutaka kurudi kwenye jamii za asili, hata kama hawatakuwa na maendeleo na ustaraabu uliopo kwenye jamii za kisasa. Watakuwa na uhuru mkubwa na maisha yao yatakuwa na maana.

Mwandishi wako,

Maureen Kemei.

kemeimaureen7@gmail.com.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *