Henry Ford aliwahi kunukuliwa akisema, kama unaamini unaweza au unaamini huwezi uko sahihi.” – Henry Ford
Kama unaamini kitu kinawezekana na mtizamo wako ni kuwa tayari kufanya chochote na kwa muda wowote kukipata, basi mafanikio kwako ni swala la muda tu.
Kwa hali hii unakuwa na uhakika wa kufikia mafaniko kwenye jambo lolote unalofanya. Unaweza kujiongezea kujiamini kwa kusoma vitabu vya kujijenga, kusoma blogu za kukufundisha na kukuhamasisha na hata kuhudhuria semina mbalimbali.
Hatua ya kuchukua leo; Amini unaweza na utaweza.
Kila kitu kinawezekana.
Kama utaweka vitu vizuri kwenye akili yako, utakuwa imara na utajiamini zaidi.
Rafiki yako,
Maureen Kemei .
kemeimaureen7@gmail.com.