Watu wengi wamekuwa wanafanya mambo kwa akili ya kujijengea sifa baada ya kuondoka hapa duniani. Wanafanya kwa lengo la kuendelea kukumbukwa vizazi kwa vizazi kwa majina yao kuandikwa maeneo muhimu au kuchongwa sanamu.
Lakini kama ilivyo mambo mengine ya maisha, unapolazimisha kitu huwa hakitokei.
Unapofanya mambo Ili ukumbukwe, hakuna anayekukumbuka, kwa sababu unakuwa siyo halisi.
Rafiki unapaswa uachane na msukumo wa kufanya vitu ili kukumbukwa au kuacha alama.
Badala yake chagua kuishi maisha halisi kwako, simamia kile kweli unachoamini na utakuwa na maisha bora huku pia ukiwa na nafasi kubwa ya kuendelea kukumbukwa.
Watu hawatakukumbuka kwa sababu unataka wakukumbuke, bali watakukumbuka kwa aina ya maisha uliyoishi .
Kuchukua hatua, wajibu wako kubwa ni kuyaishi maisha yako kwa uhalisi na ukamilifu.
Rafiki yako,
Maureen Kemei
kemeimaureen7@gmail.com.