Rafiki yangu mpendwa kama kuna kitu ambacho kinawazuia watu wengi kufanikiwa ni hofu.
Hofu imekuwa kikwazo kwa watu wengi kuchukua hatua na kuweza kufanikiwa kwenye maisha yao.
Watu wanakuwa na ndoto kubwa, wanaweka mipango mizuri, lakini inapofika kwenye utekelezaji ndipo hofu huchukua nafasi hiyo na basi watu hawaanzi.
Zipo hofu nyingi, lakini hofu moja kubwa inayoongoza kwa kuua ndoto za watu ni hofu ya kushindwa.
Hii imekuwa inawazuia watu wengi kuchukua hatua na kuweza kufanya makubwa. Hii ni kwa sababu kwa lolote kubwa ambalo mtu anapanga kufanya, ipo hatari ya kushindwa.
Ukweli ni kwamba, mambo huwa hayawi mabaya kama tunavyofikiria yatakuwa. Huwa yanakuwa kwenye hali ya tofauti na tulivyotegemea, lakini maisha bado itaendelea.
Dawa ya hofu ya kushindwa ni kuanza kidogo kidogo kabisa, kwa hatua ndogo kabisa ambayo ukishindwa hutajali au maisha yako hayatakuwa hatarini kama ulivyofikiria.
Mfano, weka lengo dogo kabisa unaloweza kulifanyia kazi kwa siku moja, alafu jifanyie tathmini, umeweza kufanya kwa kiasi gani. Wapi umefanya vizuri na wapi una changamoto.
Kisha, panga kuchukua hatua nyingine ndoto na endelea kupiga hatua hivyo kila siku, baada ya muda utakuwa upo mbali sana.Ukilinganisha na kama usingeanza kabisa.
Kwa kuanza kufanya ukianzia hatua ndogo ndogo unaiua hofu kabisa kwa sababu kwanza unajizoesha kufanya kile ambacho hujazoea kufanya na unafanya kwa ngazi ya chini kabisa.
Na pili unajijengea kujiamini kwa kuwa unafanya, tofauti na pale unaponga pekee. Unapofanya kitu na kukamilika, hata kama ni kidogo, unajijengea kujiamini na baadae utaweza kufanya kwa uzoefu ambayo utakuwa umejijengea kwa kufanya.
Rafiki, chochote unachopanga tu bila kuanza kufanyia kazi, nakushauri leo uanzie hapo kwa kufanya kwa udogo bila kuacha na utaweza kushinda hofu.
Mwandishi wako,
Maureen Kemei .
kemeimaureen7@gmail.com
uamshobinafsi.com