Uhitaji Wa Kuwa Tayari Kujaribu.

Rafiki yangu mpendwa mara kwa mara umekuwa ukipata mawazo mazuri na bora sana ambayo yana nguvu ya kuleta mafanikio makubwa.

Labda ni namna ya kufanya kazi yako kwa ubora zaidi. Au namna unaweza kuifanya biashara yako kwa viwango vya juu.

Lakini kadiri unavyoendelea kuyafikiria mawazo hayo mazuri, wasiwasi unaibuka ndani yako, unaona huwezi kuyatekeleza , kwa sababu ni makubwa na magumu.

Unaona ukijaribu utashindwa, na hapo unaamua kuachana na mawazo hayo mazuri.

Rafiki yangu hapo unakuwa umechagua kushindwa kabla hata hujaanza. Badala ya kwenda hivyo, chagua kuwa mtu wa kujaribu.

Kwa wazo lolote kubwa na bora unalokuwa nalo, hakikisha kuna hatua unachukua ili kuanza kulitekeleza. Hata kama ni hatua ndogo kiasi gani, ina uwezo wa kufungua fursa kubwa mbele yako.

Kwa kujaribu hakuna matokeo ya kushindwa. Maana kama utafanikiwa utakuwa umepata matokeo mazuri. Na kama hutakuwa umefanikiwa utakuwa umejifunza kitu ambacho hukuwa unakijua awali.

Kuchukua hatua; rafiki usikubali kupoteza mawazo mazuri yanayokujia, badala yake yafanyie kazi na hutabaki pale ulipo.

Rafiki na mwandishi wako,

Maureen Kemei.

kemeimaureen7@gmail.com.

uamshobinafsi.com

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *