Rafiki yangu mpendwa uwekezaji bora kabisa na muhimu kwenye maisha yako, tena ambao hautakugharimu ni kwenye vitabu.
Kwa gharama ndogo sana utanunua uzoefu wa watu walioishi miaka mingi na kufanya makubwa.
Hivyo kila unapopata, fanya uwekezaji huu, nunua vitabu vingi kuliko hata unavyoweza kuvisoma.
Na katika usomaji wa vitabu, jua havifanani, kuna vitabu ambavyo hutamaliza hata kuvisoma. Kuna vitabu utasoma mara moja tu. Halafu kula vitabu utarudia kuvisomaara nyingi.
Kwa vitabu bora na unavyochagua kurudia kuvisoma, mara nyingi nunua nakala nyingi za kitabu husika. Hilo litakusaidia kuwa na kitabu hicho wakati wote lakini pia utaweza kuwapa wengine kitabu hicho kama zawadi. Robin anatuambia huwa ana nakala mpaka 40 za kitabu kimoja.
Unaporudia kusoma kitabu bora, unajifunza vitu vipya ambavyo hukujifunza wakati unasoma mwanzo. Kwa sababu umekuwa mtu mpya na hivyo uelewa wako unabadilika pia.
Chukua hatua; rafiki yangu wekeza sana kwenye vitabu na chagua vitabu vichache ambavyo utakuwa unarudia kusoma mara kwa mara.
Rafiki wako,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.
uamshobianfsi.com