Changamoto 2 Kubwa Kwenye Mabadiliko Ya Tabia.

Rafiki yangu mpendwa tunapojaribu kubadili tabia, iwe ni kujenga tabia mpya au ni kuvunja tabia mbaya. Huwa tunakwama kwa sababu ya changamoto kubwa mbili.

Moja tunajaribu kubadili kitu kisicho sahihi, yaani tunachobadili siyo kinachoweza kutuletea matokeo tunayoyataka.

Mbili ni tunajaribu kubadili tabia kwa njia isiyo sahihi.

Sina uhakika kama itakufaa, lakini kwenye kubadili kisicho sahihi, huwa kuna ngazi tatu za kubadili tabia.

Ngazi ya kwanza ni kubadili matokeo, hapa mtu unahangaika kubadili matokeo. Malengo mengi huwa unawekwa kwenye ngazi hii ya kwanza.

Ngazi ya pili ni kubadili mchakato, hapa unabadili njia unayotumia kufikia matokeo. Hapa ndipo mtu unapojenga tabia.

Ngazi ya tatu ni kubadili utambulisho wako,kubadilika wewe kulingana na kile unachotaka kubadili. Hapa unabadili imani na msimamo yako juu ya kitu fulani.

Unapotaka kuleta mabadiliko ya kweli na ya kudumu kwenye maisha yako, basi unapaswa kuanza kubadilika wewe mwenyewe, kisha kubadili mchakato na hapo ndipo matokeo yatabadilika.

Watu wengi wanakwama kwenye mabadiliko kwa sababu wanakazana na matokeo, huku mchakato na utambulisho wako ukipaki vile vile.

Chukua hatua; rafiki yangu ngangana kubadilika wewe mwenyewe kisha kubadili mchakato na hapo ndipo matokeo yatabadilika.

Uwe na siku njema kutoka kwa rafiki na mwandishi wako,

Maureen Kemei.

kemeimaureen7@gmail.com.

uamshobinafi.com.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *