Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini maneno tunayotumia huwa yana maana kubwa na kuathiri sana maisha yetu.
Maneno unayotoa yanatuma ujumbe ni aina gani ya fikra zinazotawala akili yako.
Aina ya fikra zinazotawala akili yako ndiyo zitaamua kama utafanikiwa au kushindwa.
Kuna maneno hasi huwa tunayatumia kama utani kivumishi cha vitu mbalimbali.
Mfano, umefanya kazi nzuri na watu wanasema umepambana kishenzi. Au umefanya vizuri na watu kusema umeua kabisa.
Maneno ya aina hiyo, japo yanaonekana ni sifa, lakini kwa kuwa ni hasi yanaathiri matokeo yako.
Pia kuna maneno hasi tunayojiambia kwa nia nzuri tu, labda ni ndoto kubwa sana unazokuwa nazo na kujiambia haziwezekani.
Kitendo tu cha kujiambia kitu hakiwezekani, unatengeneza utabiri ambao unakuja kuwa wa kweli.
Kwa kuamini kitu hakiwezekani unaacha kuziona fursa nzuri zinazokuzunguka za kuiwezesha kuwezekana.
Kamwe usikubali kutumia maneno au fikra hasi kwenye uwezo wako, ndoto zako au matokeo unayoyataka.
Hatua ya kuchukua; rafiki tunapaswa kufuta kabisa maneno haiwezekani, mbaya, ngumu na mengine ya aina hiyo ambayo tumezoea kuyatumia na mtazamo wetu utabadilika sana.
Tutaona uwezekano kwenye kila kitu, tutaziona fursa nzuri za kufanya tunayotaka na hilo litatupa mafanikio makubwa.
Rafiki na mwandishi wako,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.