Hatua Ya 1 Kuchukua Ili Kubadili Maisha Yako.

“The moment you accept responsibility for everything in your life is the moment you can change anything in your life.” Hal Elrod.

Rafiki yangu hatua ya kwanza kuchukua ili kubadili maisha yako, ni kukubali kwamba kila kitu kwenye maisha yako ni wajibu wako.

Hapa unaondokana kabisa na kulaumu na kulalamikia wengine pale ambapo maisha yako hayaendi vizuri.

Sina uhakika kama itakufaa, lakini pale ambapo unaona maisha yako hayako kama unavyotaka yawe, basi jua hilo ni jukumu lako.

Hivyo basi, kama unashindwa, jua wewe ndiye mwenye jukumu la maisha yako.

Kama unataka kufanikiwa, jua ni wewe pekee unayeweza kujifikisha kwenye mafanikio yako.

Hata kama kuna wengine wanakukwamisha kufanikiwa, kubali hilo kama jukumu na tatizo lako, kisha chukua hatua sahihi za kulitatua ili kufanikiwa zaidi kwenye maisha yako.

Kulalamika na kuwalaumu wengine ni kujiondoa kwenye nafasi ya kufanikiwa. Kwa sababu unapolaumu mtu mwingine, maana yake unampa jukumu la maisha yako, na hakuna aliye tayari kubeba jukumu la maisha yako.

Kuchukua hatua; kama unataka kufanikiwa, kama unataka kuwa na maisha unayotaka na kuondoka kwenye maisha magumu, kubali maisha yako na kila kinachotokea kama wajibu wako, na kisha chukua hatua sahihi za kukutoa hapo ulipo sasa na kukufikisha mbali zaidi.

Mwandishi na rafiki wako,

kemeimaureen7@gmail.com

uamshobinafsi.com.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *