Jinsi Ya Kuishi Wito Wako.

Rafiki yangu mpendwa kila mtu ana wito fulani ndani yake, asili inayomvuta zaidi kufanya zaidi vitu vya aina fulani.

Sina uhakika kama itakufaa, lakini mtu anapofanya kitu cha wito wake,anafurahia anakuwa na hamasa na hachoki,anajituma zaidi katika kukifanya.

Wale wanaofanikiwa sana ni wale wanaojua wito wa maisha yao na kuuishi kwa viwango vya juu sana.

Kwa kuishi wito wako, anza kwa kuangalia vitu ambavyo ulikuwa unapenda kufanya au kufuatilia tangu ukiwa mdogo.

Kisha ingia kuvifanya kama kazi au biashara inayokulipa, huku ukiendelea kujifunza kuhusu unachofanya na kuhusu wewe mwenyewe na kuendelea kujiboresha zaidi.

Kwa kwenda hivyo, utajikuta umetengeneza kazi au biashara ya kipekee kwako inayowanufaisha watu na inayokulipa sana.

Rafiki uzuri wa kuishi wito wako ni hakuna anayeweza kushindana na wewe, akakushinda, maana hapo unakuwa unaishi maisha na siyo kuyaigiza.

Kuchukua hatua; rafiki anza kujua na kuishi wito wako ili kufanya makubwa na kufurahia maisha yako ukiwa hai hapa duniani.

Mwandishi wako,

Maureen Kemei.

kemeimaureen7@gmail.com.

uamshobinafsi.com.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *