Rafiki yangu mpendwa kutengeneza maana kwenye maisha ni matokeo ya kutengeneza utaratibu kwenye ufahamu wako.
Ni kuyaelekeza yale yote unayofanya katika kuzalisha hali ambayo inayafanya maisha yako kuwa bora zaidi.
Hatua la kwanza ni unapaswa kuwa na kusudi la maisha yako, unapaswa kuwa na kitu ambacho kinakusuma kuweka juhudi zaidi kwenye yale unayofanya kwenye maisha yako.
Kusudi lako la maisha ndiyo linalokusuma kuweka umakini wako kwenye yale unayoyafanya na hata kujituma zaidi pale unapojisikia kukataa tamaa. Kusudi la maisha ndilo linalokuwezesha kuvuka vikwazo na magumu mbalimbali tunayokutana nayo.
Mbili ni kuwa na malengo ambayo yanakufikisha kwenye kusudi la maisha yako. Kusudi lako halitafikiwa kama ajali, lazima ukae chini uweke malengo na mipango itakayokuwezesha kufikia kusudi hilo.
Malengo yako ndiyo yanayoamua wapi uweke umakini na jinsi gani utumie nguvu za ufahamu wako. Bila ya malengo utatawanya vibaya nguvu zako za ufahamu, utachoka huku ukiwa hakuna kubwa ulilofanya. Malengo ndiyo yanayotuweka kwenye mstari wa kulifikia kusudi la maisha yetu.
Tatu ni kuwa na maelewano kati ya kusudi na malengo, hili ndiyo muhimu sana kwa sababu bila ya maelewano mazuri baina ya kusudi lako na malengo unayoweka, hutaweza kupiga hatua. Lazima kila unachofanya kiwe kinachangia kwenye kufikia kusudi lako, na fikra zako ziwe kwenye unachofanya.
Rafiki, kila unachofanya lazima uweze kukielezea kinachangiaje kwenye malengo na kusudi la maisha yako.
Mwandishi wako,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.
uamshobinafsi.com.