Rafiki yangu mpendwa wanasayansi huwa wanafanya majaribio mbalimbali,wanakusanya taarifa, wanafikia hitimisho na kisha kuondoka na kile walichogundua.
Wanasayansi wanapofanya majaribio hawaanzi wakiwa na jibu fulani, hivyo wanakuwa tayari kupokea jibu lolote na kujifunza.
Rafiki, hivyo ndivyo unavyopaswa kuwa kwenye unachofanya. Iwe ni kazi au biashara, kila wakati, jaribu vitu vya tofauti, angalia matokeo unayopata kisha jifunze na boresha zaidi.
Majaribio hayo hayapaswi kuwa na mwisho hata kama umefanikiwa kiasi gani. Endeleza majaribio hayo kwenye kila fursa unayopata ama wazo lolote lile na kwa kufanya hivyo unapaswa kupima na vigezo 5 vya majaribio kama ambavyo tumejifunza kwenye somo la jana.
Chukua hatua, wewe angalia kile ambacho umeshazoea kufanya na jiulize kwamba vipi kama ningekifanya hivi. Hata kama inaonekana ni njia ya ajabu, usijipe majibu mwenyewe, fanya jaribio na utajifunza mengi ya kukuwezesha kujiboresha zaidi.
mwandishi wako,
Maureen Kemei,
kemeimaureen7@gmail.com.
uamshobinafsi.com