Mambo 5 Ya Kusema Hapana Kwenye Maisha Yako.

Rafiki tangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, ni kwenye muda pekee ndipo penye demokrasia ya kweli duniani.

Ndiyo kitu pekee ambacho wote tumepewa kwa usawa.Sasa kwa kuwa tumepewa kwa usawa, ila wapo ambao wanafanya makubwa sana kwenye muda huo huo, ina maana kuna vitu wanafanya kwa utofauti.

Na hapo ndipo muda unapokuwa muhimu sana.Na ndiyo maana muda ni kitu kingine ninachokiamini mno.

Naamini ukitumia muda wako vizuri, utaweza kufanya makubwa kwenye maisha yako.Kwa yote ambayo watu wengi wameweza kufanya, ni kwa sababu wamekuwa wanakazana kutumia muda wao vizuri.

Na siri kuu ya kutumia muda vizuri ni kusema HAPANA kwenye mambo yote ambayo hayana mchango kwenye maisha yako na mafanikio unayotaka.

Kwa mfano, haya ni mambo ambayo watu wanaofazidi kufanikiwa wanasema hapana kwenye maisha yao na kutokuyafanya kumeokoa muda wao mwingi.

1. Kufuatilia habari kwa tv, redio, magazeti na vyombo vingine vya habari.

2. Matumizi ya mitandao ya kijamii, hawatumii muda wao kuzurura kwenye mtandao wowote wa kijamii.

3. Ushabiki wa mchezo wa aina yoyote ile, huwa hawafuatilii.

4. Ulevi na starehe mbalimbali, wengi hawatumii kilevi chochote.

5. Vikao na shughuli nyingi za kijamii, shughuli ambao siyo muhimu kwako hawahudhurii.

Kwa kusema hapana kwenye hayo, wanabaki na muda mwingi ambao wanaweza kuutumia kwenye mambo yenye tija zaidi.

Rai yangu kwako rafiki yangu ni hii, linda sana muda wako. Tumia neno HAPANA kwa yote yasiyokuwa na mchango kwenye mafanikio unayoyataka.

Tahadhari;Jamii ina mbinu nyingi sana za kunasa muda wako.Inakulazimisha ufanye yale ambayo kila mtu anafanya ndiyo uonekane wa kawaida.

Chagua kama unataka kuwa wa kawaida na usifanikiwe.Au kuwa wa ajabu na ufanikiwe.

Huwezi kufanikiwa bila kuonekana wa ajabu kwenye jamii.Kwamba hufuatilii habari, haupo kwenye mitandao na hushabikii chochote!Wengi watakuona una tatizo, ila wao ndiyo wenye tatizo kubwa zaidi.

Rafiki yangu, kutoka ndani ya moyo wangu kabisa hayo ni mambo ninayoyaamini bila ya shaka yoyote ile.

Mwandishi wako,

Maureen Kemei.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *