Njia 2 Ya Kuyakabili Magumu.

Rafiki yangu mpendwa, wastoa wanatushirikisha njia kuu mbili tunazoweza kuzitumia kuyakabili magumu ili yasivuruge maisha yetu.

Njia ya kwanza ni kutambua wema pekee ndiyo kitu bora. Hapa ustoa unatukumbusha kurudi kwenye asili yetu binadamu ambayo ni viumbe wa kufikiri. Hivyo tunapaswa kuziweka fikra zetu vizuri na tusitawaliwe na hisia zozote mbaya.

Kwani kinachofanya mambo kiharibike tunapopitia magumu ni tunaporuhusu kutawaliwa na hisia.

Njia ya pili ni kutambua baadhi ya mambo yapo nje ya uwezo wetu. Kwamba tunaweza kufanya kila kinachopaswa kufanya lakini bado tutakutana na magumu kwa sababu kuna yaliyo nje ya uwezo wetu yanayokuwa yameingilia.

Ni muhimu kujua mambo yapi yapo ndani ya uwezo wetu na kuyafanyia kazi, huku yale yaliyo nje ya uwezo wetu kuyapokea kama yalivyo.

Kwa kutumia njia hizi mbili kwa pamoja, hakuna gumu lolote linaloweza kututikisa, kwani tunafikiri kwa usahihi na kujua yaliyo nje ya uwezo wetu hatuna namna ya kuyaathiri.

Hata pale magumu yanapotokea hatupati taharuki au kuumia sana kwa sababu siyo kitu kinachokuja kwetu kwa mshangao.

Rafiki Yako.

Maureen Kemei.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *