Rafiki yangu mpendwa kila unayemwona ameweza kufanya makubwa kwenye maisha yake, haikutokea kama bahati au ajali. Bali ni matokeo ya mchakato ambao mtu huyo ameufuata kwa muda mrefu.
Japo mchakato wowote hauna matokeo ya uhakika, kwa kufuata mchakato wengi wameweza kuzalisha matokeo bora.
Mchakato unahusisha mitazamo na misingi ambayo mtu anatumia kufanya maamuzi. Hapa ni baadhi ya mitazamo na misingi inayosimamiwa na wengi walioweza kufanya makubwa.
- Ujuzi siyo sawa na kipaji.
- Mchakato mzuri unaweza kuzalisha matokeo mazuri, japo siyo uhakika.
- Kutaka ukamilifu siyo mpaka uwe mkamilifu.
- Kutaka uhakika ni kujidangnya.
- Kiburi ni kunyume na uaminifu.
- Mitazamo ni ujuzi.
- Mkwamo wa kiuandishi ni kitu ambacho hakipo.
- Wabobezi wanazalisha kwa nia, siyo hisia.
- Ubunifu ni kitendo cha uongozi.
- Viongozi ni waigizaji.
- Ukosoaji wote haufanani Tunakuwa wabunifu pale tunapozalisha kazi ya kibunifu.
- Kuweza kuchagua vizuri ni ujuzi.
- Hamada ni uchaguzi.
Chukua hatua, tunapaswa kukaa kwenye mchakato kwa muda mrefu na bila shaka tunapata matokeo.
Mimi wako,
Maureen Kemei.