Mambo 10 Ya Kufanya Yatakayo Badili Maisha Yako.

Rafiki yangu mpendwa yapo mambo kumi tunayopaswa kufanya yatakayo badili maisha. Yafuatayo ni mambo hayo kumi;

  1. Kupenda ninachofanya.
    Nahitaji niwe na hamasa kubwa kwenye kile ninachofanya na kuipenda kuliko kitu chochote. Kubadili ninachofanya. Mfano kama nataka kuanzisha biashara, nikae chini na kupanga kuweka akiba, mtaji wa biashara na ya matumizi binafsi iwapo nitaacha kazi.
  2. Kubali kwamba mabadiliko yapo na yataendelea kuwepo. Ni muhimu kukubali na kukiri kwamba matokeo yanakuja, hutakuwa na mtu wa kumlaumu pale ambapo mabadiliko yatakukuta hujajiandaa.
  3. Kujifunza sana kuhusiana na unachofanya.Nijifunze sana kuhusiana na kile ambacho nakifanya.Kufanyia kazi utalaamu wako,kujua mabadiliko kwenye taaaluma yako. Kufanyia kazi eneo la kazi.

Kama unafanya biashara una majukumu mengi zaidi.

a).Unatakiwa kujijua wewe mwenyewe, kujua uwezo wako, ni vitu gani kwenye biashara yako ambavyo uko vizuri. Pia kujua ni maeneo gani haupo vizuri sana una madhaifu gani.

    Kinahitaji jitihada za ziada za kutafakari na kuchukua hatua.

    b). Ukishajua wewe mwenyewe unatakiwa kujua biashara yako vizuri, kuijua nje na ndani.

    c).Uhitaji wa kuwajua wateja wako vizuri, kujua sifa zote za mteja wako. Kujua umri wake, kipato wake, hadhi yake ya maisha, eneo analoishi na hata mahitaji yake kulingana na biashara ninayofanya.

    Litakuwezesha kujua njia za kuongeza wateja zaidi na hata pale ambapo wateja wako wanabadilika.

    d). Kujua nani ni mpinzani wako, anaweza kuwa mpinzani wa moja kwa moja au asiye moja kwa moja.

      1. Kufanya kwa ubora wa hali ya juu sana, usiweke mazoea. Kwa kufanya kitu cha ziada, kwa kuongeza ubora na thamani.Kuhakikisha hufanyi mambo kimazoea, kuhakikisha leo hufanyi kama vile ulifanya Jana.
      2. Nusa mabadiliko, kuwa mdadisi.Kuwa mdadisi, usikubali majibu ya haraka, kutokubaliana na kila kitu, kuhoji kila kitu, kujihoji mwenyewe, kutumia udadisi huu kwenye mambo chanya.
      1. Kuchukua hatua mapema.Hili kunufaika na mabadiliko ni vizuri kujua na pia kuchukua hatua ambayo itakuwezesha kuwa kwenye nafasi nzuri ya kunufaika na mabadiliko hayo.
      1. Kujua kwamba hakuna atayekuja kukutoa hapo ulipo.
      2. Kushirikiana na wengine.
      3. Kuwa tayari kusimama mwenyewe.
      4. Kubali na kusonga mbele.

      Kuchukua hatua hayo ni mambo muhimu tukizingatia na kuweka kwenye matendo tutaweza kupata kile tunachokitaka na pia kufikia malengo yetu.

      Rafiki yako,

      Maureen Kemei.

      kemeimaureen7@gmail.com

      By Maureen Kemei

      Author, psychologist.

      Leave a comment

      Your email address will not be published. Required fields are marked *