Rafiki yangu mpendwa hebu tuanzie kwa kuchunguza tabia za furaha. Kama inavyosemekana kwamba tabia tulizonazo zinaathiri sana furaha zetu.
Rafiki hapa kuna orodha ya tabia ambazo ukijijengea, utaweza kuwa na furaha kwenye maisha yako.
1. Kufanya tahajudi ( meditation).
2. Kuacha kuwalaumu wengine.
3. Kupata mwanga wa jua na tabasamu
4. Kuondokana na tamaa yoyote ile.
5. Kuachana na ulevi au vichangamsha akili kama kahawa.
6. Kufanya mazoezi ya mwili kila siku.
7. Kuwaambia wengine una furaha, kitu kitakachokulazimisha uwe na furaha kweli.
8. Kupunguza matumizi ya simu janja ( smartphone).
9. Kuepuka kuwa na siri nyingi.
10. Kusimama pale unapoteleza, mfano unapojikuta umevurugwa fanya tahajudi kurudi kwenye utulivu wako.
11. Usitegemee chochote cha nje kupata furaha.
12. Kuwa na kipimo binafsi unachojipima nacho mwenyewe na siyo kujilinganisha na wengine.
13. Kuwa na mtazamo chanya na matumaini kwenye kila jambo.
14. Epuka mchezo ya hadhi ambayo ili upande lazima uwashushe wengine.
15. Zalisha kemikali za furaha kwenye ubongo bila ya kutumia madawa ya kulevya, fanya mazoezi, kuwa na mtazamo chanya na kukaa kwenye asili.
Chukua hatua tunapaswa kujijengea na kuishi tabia hizo kila siku na tutaweza kuwa na furaha kwenye maisha yetu.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com