Mambo 28 Ambayo Nimejifunza Kwenye Safari Yangu Ya Maisha.

Rafiki yangu mpendwa, sina uhakika kama itakufaa, lakini naona bora nikushirikishe yale nimekuwa nikijifunza kwenye safari yangu ya maisha.

Ninaposherekea siku ya kuzaliwa kwangu, ikiwa leo nina miaka 28, yapo mambo mengi ambayo nimejifunza, ninapoendela kupigania ndoto ya maisha yangu ya kuwa mshauri, mwandishi na pia muuzaji bora kuwahi kutokea. Napenda kushukuru Mungu kwa uhai na uzima ambao amenijalia hadi leo.

Nashukuru pia watu wangu wa karibu ambao wamekuwa wakinishika mkono kama wazazi wangu wote mama na baba, ndugu zangu na pia mtoto wangu wa kipekee sana na marafiki wangu wote mbarikiwe sana.

Nawashukuru pia familia ya wanamafanikio hasa Kocha Makirita Amani, Songa mbele consultant na wapambanaji wote wa familia ya kisima cha maarifa KCM.

Nimejifunza mambo mengi ila baadhi ya hayo ni kama yafuatayo 28;

  1. Napaswa niwe na kusudi la maisha yangu.
  2. Kama sio sahihi nisifange, kama sio kweli nisiseme.
  3. Niwe tayari kwa mabadiliko, kwani kila kitu hubadilika.
  4. Sifai kushindwa kwenye kujifunza na kwenye kufanya kazi.
  5. Nidhamu ni kitu muhimu sana kwenye maisha.
  6. Niwe tayari kulipa gharama.
  7. Hakuna kitu cha bure chini ya jua.
  8. Nijihusishe na watu wa kuaminika kwenye maisha.
  9. Niwe mchangamfu hata kama nina matatizo.
  10. Nisiwe na chuki.
  11. Nisiwe na wivu.
  12. Nisitumie zaidi ya kipato changu na niwe naweka akiba cha asilimia kumi ya kila kipato.
  13. Nifanye yale ninayepaswa kufanya.
  14. Maisha hayafiki tamati pale ninaposhidwa, pali pale ninapokata tamaa.
  15. Elimu haina mwisho.
  16. Lazima nikae kwenye mchakato sahihi.
  17. Sifai kuwa kiranja wa dunia.
  18. Lazima niseme hapana kwenye mambo mengi.
  19. Niwe na utulivu kwenye maisha yangu ya kila siku.
  20. Nisipoendea chenye ninataka, hakitanikujia.
  21. Maisha yangu yanajengwa na kile ninachokila na kile ninachokilisha akili yangu.
  22. Niwe ninasoma angalau kitabu kimoja kila wiki.
  23. Hakuna kitu rahisi nisipoweka kazi.
  24. Nifanye tahajudi na sala kila mara.
  25. Niwe na malengo na mipango ninayofanyia kazi kila siku.
  26. Kuwa sahihi ni kukosea.
  27. Bora mtu anayetembea kuliko anayeongea.
  28. Niwe msikilizaji mzuri wakati wote.

Rafiki yako anayekupenda,

Maureen Kemei.

kemeimaureen7@gmail.com

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *