Rafiki yangu mpendwa unapokuwa na chanzo kimoja cha sauti inakupa uwezo mzuri wa kufikiri kwa kina.
Kuna wachache tu waliofanikiwa kutengeneza utulivu wao dhidi ya kelele za dunia zilizopo kila kona. Hii imewasaidia kuamsha uwezo wao halisi na kuleta mafanikio.
Jambo la kwanza; Ni kujitenga na kundi. Si rahisi kuamini upekee katika kundi. Kwa sababu kundi huamini kuwa watu wote ni sawa. Hii imekuwa sababu ya wengi kutoamsha uwezo wao halisi.
Pikli; Utulivu hukusanya nguvu, hii ni kwa sababu unasikia sauti moja tu, hivyo akili na nguvu zako zinajikita kwenye kufikiri na kutendea kazi sauti iyo moja.
Tatu; Moyo wako ndio wenye sauti yako; moyo una siri kubwa juu yake, na huu ndio kifaa cha sauti ya upekee wa maisha yako. Washa na sikiliza moyo wako ukiwa kwenye utulivu ( kujitenga na kundi).
Nne; Tenga muda wa kuwa wewe. Sina uhakika kama itakufaa, lakini kuwa wewe ni kujitenga kabisa na dunia, yaani kujitenga na shughuli na taarifa zote za dunia na kubaki wewe.
Hapo unajisikiliza mwenyewe, unajihoji mwenyewe, na kujijibu mwenyewe na kujitafakari mwenyewe ulivyo.
Tano; Kufanya tahajudi . Kwa kutafuta eneo tulivu, weka akili izingatie kwenye kile unachohitaji, kihisi kile unachokizungumzia, thibiti pumzi yako, fanya hivi kila siku. Muda mwingine unahitaji wazo moja tu ili kubadilisha maisha yako.
Hatua za kuchukua ; Unaweza tenga muda kila siku wa kutafakari kuhusu maisha yako na kuhusu wewe mwenyewe.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.