Kutoa Zaidi Kupata Zaidi.

Rafiki yangu mpendwa kuna tafiti zinaonyesha kadiri watu wanavyotoa, ndivyo wanavyopata zaidi.

Utafiti uliofanywa kwa wale wanaotoa misaada ya fedha kwa wengine unaonesha kwa kila dola moja ambayo mtu anatoa kama msaada, anapata dola 3.75 zaidi kwenye kipato chake.

Kinachowapelekea wale wanaotoa kupata zaidi ni furaha wanayoipata kwenye utoaji ambayo inawapa msukumo wa kufanya kazi kwa juhudi zaidi na hivyo kupelekea kuongeza kipato zaidi.

Utafiti mwingine umewahi kufanywa ambapo watu walipewa dola 20 na kupewa nafasi kuchagua jinsi ya kuitumia. Wale waliotumia kuwasaidia wengine walikuwa na furaha kuliko wale walioitumia kwa mambo yao binafsi. Hivyo kuwasaidia wengine kunawapa furaha zaidi.

Kuna utajiri wa tafiti unaoonyesha kwamba watu wenye furaha huwa wanafanya kazi kwa juhudi zaidi, wanafanya kazi kwa muda mrefu na kutoa matokeo makubwa na mazuri.

Furaha pia inawafanya watu kufikiri kwa usahihi na haraka na kufanya maamuzi ambayo ni bora kwenye kile wanachofanya.

Kwa wastani, watu wenye furaha wana kipato zaidi, wana ufanisi mkubwa kazini, wanafanya maamuzi bora na kwa ujumla wana mafanikio zaidi.

Chukua hatua; toa kwa kupenda mwenyewe bila kulazimishwa.

Rafiki Yako,

Maureen Kemei.

kemeimaureen7@gmail.com

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *