Madhara Ya Kufuata Mkumbo.

Rafiki yangu mpendwa kuna hali huwa zinajitokeza kwenye kundi ambapo watu wanakuwa wanafikiria kitu kimoja, hakuna anayehoji wala kukosoa pale mambo yanapoonekana hayaendi vizuri. Wanasaikolojia wanaita hali hii groupthink na imekuwa chanzo cha matatizo makubwa kwenye taasisi nyingi.

Kufikiri kwa kufuata mkumbo huwa kunachochewa zaidi na mtazamo mgando. Pale taasisi inapokuwa na kiongozi ambaye anachukuliwa kuwa na uwezo mkubwa na kuwa mwenye mtazamo mgando, kila mtu anaweka imani yake kwa kiongozi huyo na kuona kila analofanya kuwa sahihi.

Kuna mfano wa jinsi hali ya kufikiri kwa kufuata mkumbo ilivyowahi kuwa na madhara kwenye uvamizi wa siri uliopangwa na Marekani kupindua Castro wa Cuba yaani pay of pigs invasion.

Hilo lilikuwa tukio la kushindwa kwa aibu kwa taifa hilo kubwa dhidi ya taifa dogo na uchunguzi unaonesha kilichopelekea uvamizi huo kushindwa ni watu kuacha kufikiria kwa usahihi na kufuata mkumbo.

Chanzo kikuu cha kushindwa kwa uvamizi huo ilikuwa ni kiongozi wa wakati huo, Rais Kennedy ambaye alikuwa amejijengea sifa ya kufanya mambo mengi kwa usahihi. Watu walimwamini sana na kuona ana maono makubwa na yaliyo sahihi, ambayo hayapaswi kuhojiwa wala kukosolewa.

Hivyo alipopendekeza uvamizi wa Cuba, japo mpango haukuwa sahihi, washauri wake wote walikubaliana na yeye. Yeye alifikiri wanakubaliana naye kwa sababu ya mpango, kumbe wanakubaliana naye kwa sababu ya imani waliyonayo kwake.

Kilichotokea ni uvamizi kushindwa vibaya kwa sababu ya watu kufuata mkumbo kwenye kufikiri

Chukua hatua; rafiki tunapaswa wakati wote tusikilize kundi wanasema nini, lakini kwenye kufanya maamuzi ni sahihi kufikiri kwa kina kabla ya kufanya maamuzi yoyote yale.

Rafiki yako,,

Maureen Kemei.

kemeimaureen7@gmail.com

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *