Rafiki yangu mpendwa karibu sana tujifunze kutoka vitabuni, leo nimebahatika kusoma kitabu hiking kizuri, karibu nikushirikishe.
1.Ili kufanikiwa unatakiwa kufanya vitu bila kuogopa changamoto ambazo zitatokea pamoja na kuishinda hofu katika maisha.
2. Kuna maumivu ya aina mbili moja ni maumivu ya kuikabili hofu leo ni ndogo ukilinganisha na maumivu utakayoyapata utakapo gundua hauna nguvu, muda na uwezo wa kufanya ambacho ulikuwa unakitamani kila siku .
3. Lazima kuchukua hatua leo na ufanye unachotakiwa kufanya ili baadae usijute.
4. Tunatakiwa kujifanyia tathimini kila siku katika maisha pamoja na kuacha kuishi kwa mazoea.
5. Nimejifunza kutokata tamaa pamoja na kujipa moyo pale unapoona umekata tamaa unatakiwa kutambua kwamba umefanya kazi kwa asilimia 40% tu hivyo unatakiwa kujilazimisha kufanya tena kwani kuna asilimia 60% bado hujazifanyia kazi hivyo unatakiwa kujipa moyo na kuendelea kufanya kazi zaidi .
6. Badala ya kulalamika na kulaumu pamoja na kunungunika unatakiwa kuvunja mipaka uliyojiwekea na amini kuwa unaweza kufanya na kupata unachotaka .
7. Kuna vita nyingi huwa zinaibuka katika kila unapokaribia kufanikiwa hivyo unatakiwa kutumia hekima kuchagua vita ya kupigana nayo na nyingine ambazo hutakiwa kupigana nazo .
8. Kuepuka watu walioshindwa katika maisha kwani walioshindwa wanatamani na wewe ushindwe kama wao walivyoshindwa hivyo unatakiwa kuwa makini sana na watu hao.
9. Lazima kufuatilia ndoto yako hata bila kuogopa hofu ya kutokubalika au kutokubaliana na wewe.
10. Katika jambo lolote unalotaka kufanya lazima kupambana kwa moyo wote bila kuchoka wala kukata tamaaa kikubwa kujiamini na kuamini njia yako kuwa ni sahihi pambana mpaka mwisho utapata matokeo mazuri tu.
Chukua hatua; rafiki yangu tuchukue hatua ya kupambana ndoto yetu baada ya kusoma na kuelewa mambo haya kumi.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.