Rafiki yangu mpendwa pata picha kwenye kila eneo la maisha yako, kila jambo unalofanya una bahati ya kufanikisha. Sio tu bahati unakujia hivyo tu, bali kuna vipengele muhimu unayopaswa kuzingatia.
Hapa kuna vipengele kumi ambayo tunapaswa kuzingatia kwenye maisha.
- Ukiwa na pesa kwenye maisha hata kama umri umeenda bado utaonekana kuwa kijana.
- Kwenye maisha tusijilinganishe na wengine bali tupambane kutafuta mali ili tufurahie maisha yetu ya baadaye.
- Tujifunze kwa wengine waliofanikiwa ili na sisi tufanikiwe.
- Tujifunze kutunza siri hata iwe nzito kiasi gani.
- Tusijiingize kwenye vitu ambavyo vinatuletea matatizo kwenye maisha yetu kama vile kamari na pombe.
- Tusitegee kufanya kazi. Mtu hawezi fika popote kwa kutegea kazi.
- Tupende kufanya kazi kwa ufanisi zaidi. Hakuna rafiki mzuri kama kazi. Jitahidi uipende kazi usijali hata kama ni ngumu kiasi gani.
- Mtu anayetaka kujenga nyumba nzuri hatawaza sana juu ya uzito wa nguzo au umbali wa kufuata maji ya kujengea.
- Tuthamini kazi tunayofanya. Kumbuka kuwa kazi ikifanywa vizuri inamnufaisha anayeifanya.
- Fanya kazi ili kujipatia kipato uweze kununua uhuru wako.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.