Hatua Za Kuzingatia Ili Kupunguza Msongo WA Mawazo (sehemu ya pili).

Rafiki yangu mpendwa karibu twendelee kujifunze zaidi kuhusu njia hizi za kupunguza msongo wa mawazo ili tuweze kuishi maisha ya furaha.

Haya ni baadhi ya njia za kupunguza msongo wa mawazo.

5. Udhibiti wa muda. Kuwa na wakati mzuri wa kupanga majukumu hili kupunguza hisia za kuvurugikana na kuahirisha mambo. Gawa kazi kubwa kuwa sehemu ndogo na weka vipaumbele kwa kuainisha uta anza na kipi na kuishia na kipi, hili litakusaidia kudhibiti muda vizuri.

6. Msaada wa kijamii. Wakati huu unahitaji watu wa karibu ili wakusaidie, kuwa na uhusiano mzuri na watu wa karibu husaidia kupunguza msongo wa mawazo. Kuzungumza na marafiki au familia hutoa fursa ya kushiriki hisia zako na kupata mawazo tofauti.

7. Kuimba. Uimbaji ni tiba ambayo wengi hawaitambui, jiunge na kwaya kanisani au kikundi cha uimbaji kanisani. Sikiliza wimbo ulio tulia usio na midundo mingi, muziki mtulivu ni tiba, husaidia kupunguza mvutano wa mwili na akili. Mbinu hizi hutuliza mwili na kusaidia kudhibiti kiwango cha mawazo.

8.Jihusishe na burudani sahihi. Kufanya shughuli unazozipenda, kama vile kusoma au kuchora, husaidia akili kupumzika na kuondoa mawazo ya msongo. Hata shughuli ndogo hutoa nafasi ya kufurahia wakati wa sasa na kupunguza mawazo ya kupindukia.

9. Weka mipaka. Kujifunza kusema hapana kunasaidia kuzuia kuchukia majukumu mengi kupita kiasi ambayo kusababisha msongo wa mawazo. Kujua mipaka yako ni muhimu kwa kudhibiti mzigo wa kazi.

10.Punguza muda wa vifaa vya digitali. Muda mwingi kwenye mitandano wa kijamii au skrini za simu unaweza kuongeza msongo kwa kulinganisha maisha yako na ya wengine au kwa sababu ya habari za kusumbua. Kupunguza muda wa skrini husaidia akili kupumzika.

Chukua hatua; rafiki tunapaswa kuzingatia hayo hili kupunguza msongo wa mawazo.

    Rafiki yako,

    Mauree Kemei.

    KEMEIMAUREEN7@GMAIL.COM

    By Maureen Kemei

    Author, psychologist.

    Leave a comment

    Your email address will not be published. Required fields are marked *