Rafiki yang mpendwa karibu siku ya leo tunajifunza kuhusu dalili Za kujua kama umeathirika na msongo wa mawazo.
Dalili hizi ni kama zifuatazo;
- Kuchoka akili na mwili. Mtu mwenye msongo wa mawazo anaweza kujiskia mchovu kila wakati, hata baada ya kulala au kupumzika. Ni kama mwili na akili vinakosa nguvu za kufanya shughuli ndogo kila siku.
- Wasiwasi na huzuni ya wa kwa mara. Mtu anakuwa na hali ya wasiwasi wa kudumu, ambapo anahisi kuwa mambo hayaendi sawa au kuna hatari inayoikabili, hata kama hakuna msingi wa hofu iyo. Huzuni inakuwa sugu, na mtu anaweza kupoteza hamu ya kufanya mambo aliyokuwa akiyafanya hapo awali.
- Kubadilika kwa hamu ya kula. Watu wanaokumbwa na msongo wa mawazo mara nyingi hupata mabadiliko ya hamu ya kula chakula. Wengine wanaweza kupoteza kabisa hamu ya kula, wakati wengine wanakula kupita kiasi kama njia ya kupunguza mawazo.
- Kushindwa kulala vizuri ( insomnia). Moja ya dalili Za kawaida ni shida ya kulala au kupata usingizi hafifu. Mtu anaweza kupata taabu kulala, kuamka usiku mara kwa mara, au kuamka mapema sana bila uwezo wa kurudi usingizini.
- Kushuka kwa nguvu na Ari ya kufanya kazi. Msongo wa mawazo huathiri uwezo wa kufanya kazi au kufurahia mambo ambayo awali yalikuwa yanavutia. Mtu anaweza kupoteza motisha ya kufanya kazi au shughuli za kila siku hali hii ikiambatana na hisia ya kutokujali au kutoona thamani ya juhudi zake.
- Kusumbuliwa na mawazo mbaya. Msongo wa mawazo unaweza kusababisha mawazo hasi ya mara, kama vile kujiona huna thamani, kukosa matumaini, au hata kufikiria kujiua.
- Dalili za kimwili ( maumivu ya kichwa na mwili). Mara nyingi, msongo wa mawazo unajidhihirisha kupitia maumivu ya kimwili kama vile maumivu ya kichwa, tumbo, au mgongo bila sababu ya kiafya inayoeleweka.
- Kujitenga na watu wengine. Watu wenye msongo wa mawazo wanaweza kujikuta wakiepuka mikusanyiko ya kijamii au hata watu wa karibu kwa sababu ya kutokuwa na Ari ya kushirikiana au hisia ya kuwa mzigo kwa wengine.
- Kupunguza kwa umakinifu. Msongo wa mawazo unaweza kuathiri uwezo wa mtu wa kufikiria kwa umakini, kufanya maamuzi sahihi, au kuzingatia kazi. Mtu anaweza kusahau mambo kwa urahisi au kuwa na shida ya kumaliza kazi aliyoanza.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.