Rafiki yangu mpendwa habari njema ni kwamba siku ya leo tuna bahati nzuri kabisa, na bahati iyo ni hii hapa. Kwamba leo nakushirikisha jinsi ya kuongeza bahati kwenye maisha yako.
Usiwe na wasiwasi wowote kwa maana falsafa hii imekuwapo tangu ni falsafa ya kutokudharau kitu chochote na pia kutokuamini kitu chochote.
Mwanafalsafa Epictetus anatukumbusha kutoka Kitabu chake mambo ya kufanya ili tuongeze bahati kwenye maisha yetu.
Baadhi ya mambo hayo ni kama yafuatayo;
- Mara zote fikiria kuhusu kifo na kamwe hautadharau chochote wala kutamani chochote kupitiliza. Unapofikiria kuhusu kifo kuwa ni kitu ambacho kipo, utakuwa unajua sio jambo bora kungangania vitu ambavyo hazileti manufaa kwenye maisha yako. Utajua ni swala la muda mfupi tu. Kujikumbusha kuhusu ufupi wa maisha unaweza kuendea maisha bila hofu wowote, kwa sababu unajua hata ukiogopa mwishowe utakufa na ni bora kudhubuthu kufanya jambo kuliko kukaa bila kufanya chochote.
- Unapobadili maisha yako, kwa mfano kuanza biashara, kufanya uwekezaji, kuongeza masomo au kuwa hata bilionea. Watu wengi hawatafurahishwa na hayo. Wataanza kusema unajifanya, au unajiona wewe ni bora kuliko wengine wote ama unajiona unaweza zaidi. Unachopaswa kufanya ni kuendelea kufanya kile unachokifanya bila kuruhusu wengine wakukatishe tamaa, kwani mwishowe utakapofanikiwa watakuwa wa kwanza kufurahia mafanikio yako na watakuheshimu. Unapoacha sasa kupambania matamanio yako, na kusema kuwa watu hao wanakusema vibaya, wanaona unajifanya, mwishowe ukifeli au usopofanikiwa, watu hao watakudharau zaidi na kusema wewe ni mvivu au haufai kabisa. Muhimu hapa ni kutokusikiliza kelele zao unapopambania mafanikio yako.
- Unapotaka kufanya kitu ili uonekane na wengine, tayari umeshapoteza. Kwani kuna watu tu hawatafurahia kile unachofanya. Kuwa kile ambacho unataka kuwa wewe, alafu wao watachagua kama watakubaliana na wewe au waende kinyume na wewe.
- Tusifanye maisha yetu kuwa ngumu zaidi kwa kutaka kuheshimiwa na wengine. Yote tunayohangaika nayo hatupaswi kufuatilia wengine wanasema nini. Wajibu wako ni kuwa wewe, kufanya yale muhimu kwako. Kutaka kujua wengine wanakuchukulia vipi viko nje ya uwezo wako.
- Kuhusu matokeo ambayo wengine wanapata au mafanikio ya wengine. Wengine wamefika na sisi hatujafika kama tunaona watu wamepiga hatua fulani, ni kwa sababu kuna gharama ambao wamelipa ambao sisi hatujalipa. Kwa kila mafanikio ambao tunataka kufikia kwenye maisha tunapaswa kuwa tayari kulipa gharama yoyote ile.
- Kitu ikitokea kwa wengine tupo tayari kuwatia moyo, au kuwashauri kwa mfano mtu akipoteza mpenzi wake au mmoja wa familia wake, ni rahisi sana kuwatia moyo, lakini inapokuja kwetu tunaona ni ngumu sana kuelewa kuwa imetokea na hivyo huwa inatuumiza sana. Tunapaswa kuelewa na kujua kuwa ni sehemu ya asili na inapita na maisha lazima iendelee.
- Hakuna kitu kibaya kinachotokea kwa asili hapa duniani au kikitokea ni kitu chanya au kitu kizuri. Huwa ni chema kwa ajili ya Dunia nzima, chenye manufaa, huwa ni kitu chenye manufaa kwa dunia hii. Tukijua hilo tutaweza kukabili mambo yanayotokea kwa njia nzuri zaidi.
- Ni mara ngapi umewapa watu nafasi ya kuathiri maisha yako? Sina uhakika kama itakufaa, lakini mara nyingi tunaruhusu wengine waharibu rasilimali zetu muhimu kama muda, akili zetu na nafsi zetu. Tunafanya hivyo kwa kushindwa kijiheshimu sisi wenyewe. Kwa kuruhusu watu watuvuruge na hivyo tunashangaa mbona hatupigi hatua kwenye maisha yetu. Tunaruhusu watu watupe uchafu zao ndani zetu kwa kusikiliza habari mbaya, habari hizi huondoa amani na utulivu ndani yetu na kutupa wasiwasi wa muda wote. Habari hizo ni za kutufanya tuishi kwa hofu kila mara, hivyo huathiri fikra zetu kwa sababu watu hawatakuwa na utulivu wa kifikiri kwa kina kabla ya kufanya maamuzi.
Chukua hatua; rafiki mbira iko upande wetu sasa tuhakikishe tunasoma na kuelewa falsafa hizi na kuweka kwenye matendo ili tuweze kuishi kama wastoa na kuwa wa tofauti kwenye jamii.
Rafiki yako,
Maureen Kemei
KEMEIMAUREEN7@GMAIL.COM