Kwa Nini Hufai Kuahirisha NdotoZako?

Rafiki yangu mpendwa kila mtu ana ndoto kubwa kwenye maisha yake. Kuna picha ambayo kila mtu anayo ya namna maisha yako yanataka yawe.

Lakini kwa bahati mbaya sana, wengi wamekuwa wakiahirisha ndoto zao kila wakati.

Wakijua kabisa wanapaswa kufanya nini, lakini wanaahirisha na kujiambia hawajawa tayari au muda bado.

Tunajua jinsi ambavyo hatuna muda wa uhakika hapa duniani. Na tunajua jinsi wengi wanavyokuja kujuta maisha yao yanapofika ukingoni.

Sina uhakika kama itakufaa, lakini hatupaswi kuwa hivyo, hatupaswi kuwa watu wa kuahirisha ndoto zetu. Badala yake tuzitekeleze ndoto zetu kama tunavyoziona kwenye akili zetu.

Hata kama wengine hawatatuelewa, tufanye kile tunachojua ni sahihi, maana kama ni majuto sisi wenyewe tutayapata.

Kwani muda tulionao ndiyo huu, hakuna wakati tutakuwa tayari zaidi ya tulivyo sasa.

Hatua ya kuchukua; rafiki anza kuishi ndoto zako sasa, kwa pale ulipo na kwa kile ulichonacho sasa. Hiyo ndiyo njia ya kuishi maisha kamilifu kwako.

rafiki yako,

Maureen Kemei.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

1 comment

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *