Rafiki yangu tabia ya ughairishaji mambo ni tabia ambayo inapelekea mafanikio ya mtu kuishia njiani au kufa kabisa, watu wenye tabia hii ni watu ambao huwa wanaanza upya kila siku mambo yao hawana muendelezo wa mambo waliyoyaanza.
Mtu kama huyu ni ngumu sana kumkuta amepiga hatua kwenye malengo yake na siyo kwamba hana muda kabisa au rasilimali fedha na watu la hasha ni tabia ambayo amejijengea yeye mwenyewe pasipo kujua inamvuta nyuma asiweze kufika kwenye ndoto zake.
Utajuaje una tabia hiii, yafuatayo ni mambo manne yatakayotusaidia kujua.
1. Kila kitu unakiona hakiwezekani.
2. Husimamii vilivyo kile ulichozungumza na kukipangilia.
3. Ukitengwa na marafiki zako, basi mipango yako nayo unaacha kufuatilia unaanza kutafuta kwa nini wamekutenga.
4. Unakuwa ni mtu wa kukuza changamoto sana. Ukiumwa kidogo tu hata kama ni mafua basi unaanza unakuza ugonjwa, unaghairisha mipango yako yote.
Chukua hatua; rafiki weka tabia ya kuhakiksha kila jambo ulilolipanga unalifanikisha kwa wakati hata kama itatokea changamoto wewe pambana mpaka ulikamilishe.
Makala haya nimeandika kwa ajili yangu na wewe pia rafiki yangu ambaye una tabia hii pia.
Naahidi kubadilika kwa kuchukua hatua haraka bila kughairisha mambo.
Asante.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.