Namna Ya Kujua Kuwa Unaambatana Na Marafiki Wabay( bad company).

Rafiki yangu kuna msemo unasema hivi “Nionyeshe marafiki zako nami nitakuambia tabia yako.

Marafiki wana uwezo wa kujenga hatima yako au ndoto yako au wakaua kabisa ndoto yako.

Sina uhakika kama itakufaa, lakini watu waliofanikiwa sana kwenye dunia hii ukiwafuatilia ni kwamba waliambatana na watu sahihi ambao waliwasaidia na kuwaonyesha njia sahihi za kufanikiwa hata kama walikutana na changamoto bado marafiki hao hao waliwabeba na kuhakikisha wamefika kwenye ndoto zao.

Mara nyingi ni bora kubaki mwenyewe na Mungu wako kwenye safari ya ndoto yako kuliko kuambatana na marafiki wabovu wasioelekea kule unakoelekea wewe.

Hapa mna njia nne za kujua kama una tabia hii ya kuambatana na marafiki wabovu.

  1. Muda wote unakuwa nao, wao ndio maamuzi wenye maamuzi juu ya maisha yako na siyo wewe.
  2. Unawasikiliza kwa kila kitu hata uwe ushauri mbaya utawasikiliza tu.
  3. Unaamini zaidi kwenye matendo yao.
  4. Unawapa kipaumbele kwa kila kitu, hata ukipata hela watu wa kwanza kujua ni hao marafiki zako.

Rafiki kitu cha muhimu sana cha kukusaidia kutoka kwenye tabia hii ni kuamua kutoka, unapoamua inakupa nguvu ya kutoka kwao .

Pili, ni kuanza kujitoa taratibu kwa marafiki wenye tabia zisizofaa.

Chukua hatua jijengee tabia ya kukaa na watu bora na sahihi ili uweze kufika kwenye ndoto yako.

Ukiona inakushinda sana Muombe Mungu akutenge na watu ambao siyo sahihi juu ya ndoto yako na akupe watu sahihi juu ya ndoto yako utaona urahisi na uwepesi kwenye safari ya ndoto na utafanikiwa hata kama usipofika kabisa kwenye mafanikio basi utakuwa karibu na mafanikio yako.

Usishangae mara kuona yanatokea mambo kama haya, mara hawakutafuti tena, mara unazuka tu ugomvi mnagombana na mnaachana, mara wanaanza kukusema vibaya na kukuona wa hali ya chini kuliko wao, tafadhali usijiskie vibaya kwa wakati huo tambua uko kwenye kipindi cha mpito na upo karibu sana kukutana na watu sahihi.

Marafiki watakujenga au watakubomoa ni jukumu lako kuchagua watu sahihi juu ya ndoto yako.

Rafiki yako,

Maureen Kemei.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *