Rafiki yangu mpendwa Kutokusamehe ni mlango ambao unafunga mafanikio, baraka na ndoto yako hapa duniani.
Aliyewahi kuwa Raisi wa Afrika Kusini Nelson Mandela aliwahi kupitia kipindi kigumu sana kabla ya kuwa Rais ya Nchi hiyo. Moja ya vipindi vigumu alivyopitia ni kufungwa jela kwa miaka 27.
Na kipindi yupo gerezani wale askari walikuwa wakimfanya dhihaka sana kwa kutumbukiza kwenye shimo na kumkojolea na kumwambia meneno mabaya ya kwamba hataweza kuja kuongoza Nchi ya Afrika Kusini.
Lakini wakati anakojolewa Nelson Mandela alimwambia yule askari ya kwamba siku moja nitaiongoza Nchi yangu. Na baada ya kutoka gerezani aliwasamehe wote waliomfanyia mabaya yale, na mwishowe alikuja kuiongoza Nchi kwa ushindi mkubwa.
Watu wanaweza kukukosea mambo makubwa sana na ukajisemea moyoni kwamba hutawasamehe, ukweli ni kwamba wewe ndiye utakayejiumiza na kujirudisha nyuma sana, utabeba uchungu, visasi na mwishowe ikakupelekea kutokuwaza wala kufikiria juu ya hatima ya maisha yako
Yule aliyekukosea anaweza asigundue amekukosea sana, na anaweza asikuombe hata msamaha na akaamua kukaa kimya, kwa wakati huo unatakiwa uchukue hatua ya kumsamehe na kuendelea na mambo mengine na siyo kushikilia kama ni kanuni ya mafanikio.
Utajuaje Una Tabia Ya Kutokusamehe.
- Muda wote unazunguka ubaya wa nyuma ambayo ulishawahi kufanyiwa na marafiki, mchumba, wazazi, ndugu, wafanyakazi wenzio na bosi wako hiyo ni dalili ya kwamba hukusamehe bado unatembea na mabaya hayo.
- Huamini kama kuna watu wema na wenye kutenda wema.
- Kutoshirikiana au kumsaidia yule aliyekukosea hata kama ameshaomba msamaha.
- Kukumbushia yale mabaya ya mwenzio kila wakati hata kama alishakuomba msamaha, na hii huwa inatokea sana kwa wapenzi, wachumba na Wana ndoa.
- Kupanga mabaya na visasi juu ya aliyekukosea.
Chukua hatua; tujifunze kusamehe na kuachilia siku zote za maisha yetu hapa duniani.
Rafiki Yako,
Maureen Kemei.