Rafiki yangu mpendwa maandiko yanasema hivi kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe nyinyi.
Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe nyinyi makosa yenu.
Utatoka kwenye tabia hii ya kutokusamehe kwa kufanya yafuatayo;
- Kujifunza kusamehe na kuachilia siku zote za maisha yako hapa duniani.
- Kama mtu amekukosea jambo kubwa muite kaa naye chini ongea naye kwa upendo bila kupayuka payuka kama mtu asiye na akili, mwambie mahali ambayo amekukosea, mtangazie msamaha hapo hapo na endelea kumpenda na kumtakia mema siku zote.
- Baada ya kusamehe mtu usiizungumzie tena hilo jambo, endelea na maisha yako na malengo juu ya ndoto yako.
- Tafuta kuwa na Amani ndani ya moyo wako, jifunze mambo mazuri juu ya ndoto yako.
- Jiepushe na marafiki wagomvi na wenye kupenda mapambano ya maneno.
- Siku zote kuwa mtu wa kulingana na imani yako.
Chukua hatua; rafiki katika kusamehe utaishi maisha yenye amani na furaha na itakusaidia kufika kwenye ndoto yako.
Kitu kimoja zaidi kusamehe ni mlango wa kufika kwenye ndoto yako.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.