Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini kuweka bajeti inakusaidia kufanikisha mambo mengi ya kifedha kama; kuweka malengo, kujenga nidhamu yako ya kifedha, inakusaidia kuepuka madeni ya kiholela holela, unakuwa na picha kamili ya kile ambacho kitatumika na na kuona halisi ya kifedha.
Hapa kuna mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa kuandaa bajeti.
- Lazima uangalie kipato chako halisi.
- Utajua kipato chako ni kiasi gani.
- Kutambua matumizi ya dharura ni vigumu mwezi uishe bila dharura.
- Andika bajeti yako sasa. Andika kwenye simu yako, note book yako, group private kwenye simu yako.
- Kuanza kufuatilia mwenendo wa bajeti yako, kila siku kila wiki.
- Kukitokea mabadiliko yanatokeza uzingatie pia. Mfano mapato yakiongezeka matumizi yasiongezeke.
- Kuwekeza . Mpango wa uwekezaji uwepo
- Kuepuka matumizi ya hadharani. Kushindana na watu wengine kwa mfano kununua magari, kufanya biashara, n.k.
- Jifunze kutoka kwa wengine. Soma mambo mbalimbali ili uweze ujifunza kutoka kwa wengine.
- Kagua bajeti yako mara kwa mara.
Chukua hatua; rafiki ukiwa una bajeti inakukubusha kuwa ili halikuwa kwenye bajeti yangu. Lakini bila bajeti pia fedha hazionekani, hivyo ni muhimu kuwa na bajeti.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.