Rafiki yangu mpendwa karibu sana asubuhi hii ya leo tujifunze mbinu bora za kuweza kutumia muda tulionao humu duniani vipasavyo.
Hapa kuna mbinu kumi ya kuboresha matumizi ya muda.
- Weka vipaumbele. Amua shughuli muhimu zaidi kwa siku yako na zifanye mapema kabla ya kazi zisizo za lazima.
- Tumia ratiba au kalenda. Panga shughuli zako kwa saa au kwa siku, ukihakikisha unafuata mpango huo kwa umakini.
- Epuka kuahirisha. Fanya kazi zako mara moja badala ya kuziarihisha. Kuahirisha kunapoteza muda na kuongeza msongo wa mawazo.
- Weka mipaka kwenye usumbufu. Zima arifa zisizo za lazima kwenye simu au kompyuta yako ili kuepuka kuvurugwa.
- Jifunze kusema ‘hapana’. Usikubali kila ombi au shughuli kama haichangii malengo yako au inaingilia ratiba yako.
- Fanya kazi kwa vipindi vya muda. Tumia mbinu kama, pomodoro technique, fanya kazi kwa dakika 25, kisha pumzika kwa dakika 5.
- Unda orodha ya kazi( to do list). Andika kila kitu unachohitaji kufanya kwa siku, kisha tandika kazi moja moja kwa kufuata mpangilio wa umuhimu.
- Fanya kazi kwa ufanisi zaidi. Badala ya kufanya kazi kwa muda mrefu, zingatia kumaliza haraka bila kupoteza ubora.
- Tumia teknolojia ya kurahisisha kazi. Tumia zama za kidigitali kama (task managers) au (reminders) ili kufuatilia shughuli zako.
- Jali muda wa kupumzika. Tengeneza muda wa kupumzika na kujifurahisha. Kupumzika vizuri kunaongeza uzalishaji na nguvu za kufanya kazi kwa ufanisi.
Chukua hatua; muda ni rasilimali ambayo haiwezi kuhifadhiwa au kuongeza. Tunapaswa kutumia muda vizuri kwa manufaa yetu sisi wenyewe.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.