Mambo 10 Ya Kujifunza Kutoka Kwa Maisha Ya Warren Buffett.

Rafiki yangu mpendwa karibu sana leo tunajifunza kuhusu mmoja wa wawekezaji maarufu duniani Warren Buffett.

Mambo hayo kumi ni kama yafuatayo;

  1. Uwekezaji Wa Akili Na Muda. Warren anasisistiza kujifunza na kuelewa kabla ya kuwekeza. Alisema: “usiwekeze katika kitu ambacho hukielewi ambacho hukielewi”. Anasoma sana vitabu na taarifa za kifedha kabla ya kufanya maamuzi.
  2. Kuishi Kwa Unyenyekevu. Licha ya kuwa tajiri sana, Buffet anaishi maisha ya kawaida. Anaishi kwenye nyumba aliyoinunua mwaka1958 na hana anasa nyingi. Hii inaonyesha umuhimu wa kuwa na nidhamu ya kifedha.
  3. Uvumilivu Na Mtazamo Wa Muda Mrefu. Buffet huwekeza kwa mtazamo wa muda mrefu. Alisema “soko la hisa ni chombo cha kuhamisha pesa kutoka kwa wasio na subira kwenda kwa wenye subira.”
  4. Kujifunza Kutokana Na Makosa. Buffet anakubali makosa yake ya uwekezaji na hujifunza kutokana nayo. Hili linamfanya kuwa mwekezaji bora zaidi kwa muda.
  5. Thamani Ya Mahusiano. Anasema urafiki na familia ni muhimu zaidi kuliko pesa. Anatilia mkazo maadili na ushirikiano mzuri na watu.
  6. Kuwekeza Katika Wewe Mwenyewe. Buffet anaamini kwamba kujifunza n kuboresha ujuzi wako ni uwekezaji bora zaidi. Alisema “ Uwekezaji muhimu zaidi unaweza kufanya bu katika wewe mwenyewe”.
  7. Kuokoa Na Kuwa Na Bajeti. Anaamini katika kuweka akiba na kutumia pesa kwa busara. Hii inaonyesha umuhimu wa kudhibiti matumizi na kuwa na mpango wa kifedha.
  8. Kujua Thamani Ya Muda. Buffet huchagua kufanya mambo yenye thamani kwa muda wake. Huchagua kutokuwa na a ratiba iliyojazwa sana ili kufikiria na kufanya maamuzi makubwa.
  9. Kutoogopa Kufuata Njia Tofauti. Buffet mara nyingi hufanya maamuzi yanayojipanga na mtazamo wa wengi . Alisema: “uwe na hofu wakati wengine wanakuwa na uchoyo, na uwe na uchoyo wakati wana hofu”.
  10. Kuwa Mwaminifu. Anasisitiza umuhimu wa uaminifu na maadili katika biashara na maisha. Anaamini kwamba heshima inajengwa kupitia uaminifu.

Chukua hatua; Maisha ya Warren Buffett yanatufundisha kuwa nidhamu, maarifa, na maadili vinaweza kuleta mafanikio ya muda mrefu, si tu katika fedha bali pia katika maisha kwa ujumla.

Rafiki yako,

Maureen Kemei.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *