Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini leo tunajifunza mawazo kumi ya kuboresha mchakato wa kuweka malengo.
- Tumia Mfumo Wa SMART: Hakikisha malengo yako ni mahususi (special), yanayopimika ( Measurable), Yanayoweza kufikiwa ( achievable), yanayohusiana ( relevant), na yenye kipindi maalum ( time boud).
- Gawanya malengo makubwa: Vunja lengo kubwa katika hatua ndogo ndogo ili lisionekane gumu kufanikisha.
- Andika Malengo Yako: Kuandika malengo husaidia kuyakumbuka na kuyapa kipaumbele.
- Weka Kipaumbele: Jua malengo gani ni ya haraka na muhimu zaidi, kisha uyape nafasi ya kwanza.
- Pima Maendeleo Yako Mara Mara: Chukua muda kila wiki au mwezi kitathmini jinsi unavyosonga mbele.
- Weka Kipimo Cha Mafanikio: Eleza wazi matokeo unayotarajia na jinsi utakavyopima ikiwa umeyafikisha:
- Epuka Kuweka Malengo Mengi Sana: Zingatia malengo machache ili uelekeze nguvu na rasilimali zako vizuri.
- Tafuta Usaidizi Au Ushauri. Jadili malengo yako na mtu unayemwamini ili kupata maoni na msaada wa ziada.
- Adhibu Au Zawadia Nia Yako: Jipe zawadi unapopata mafanikio madogo, au weka adhabu ndogo kama njia ya kujihamasisha.
- Jifunze Kutoka Kwa Kushindwa: Ukishindwa kufanikisha lengo, chunguza sababu, jifunze, na rekebisha mchakato wako ili kuboresha siku zijazo.
Chukua hatua; rafiki hakikisha unajitahidi kuwa thabiti na kuzingatia lengo la muda mrefu.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.