Rafiki yangu mpendwa leo tunajifunza kuhusu mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa kutoa huduma bora kwa wateja.
Mambo hayo ni kama yafuatayo;
- Kujifunza kujua mahitaji ya wateja. Kwa kuuliza maswali litasaidia kuhudumia vizuri wateja.
- Kuwa na lugha nzuri ya mwili na maneno, tumia lugha ya heshima inayojenga mahusiano na watu.
- Kutoa huduma ya haraka na ufanisi. Watu wanahitaji uharaka, mtu wa kupokea wateja kuwasaidia kusubiria kama kuangalia tv, gazeti au pipi.
- Kuzingatia maoni ya wateja; kama mmiliki wa biashara, tenga muda wa kupitia wateja wako.
- Kujenga uaminifu; hakikisha unatekekeza ahadi zako kwa mfano kama kutoa offers.
- Kuwa na muonekano mzuri; Watu wananunua wewe kabla ya bidhaa zako k.m. nywele, mavazi zako.
- Kumfuatilia mteja; Kama huduma aliyopata ameifurahia n.k. kama ana maoni kuhusu huduma yako ili waweze kurudi tena.
Chukua hatua; huduma bora kwa wateja inajenga uaminifu, mahusiano mazuri, na jina zuri la biashara.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.