Rafiki yangu mpendwa hasira ni asili ya binadamu ila inatupasa tujidhibiti. Hisia zikiwa juu uwezo wa kufikiri unakuwa chini.
Tunapaswa kukabiliana na changamoto yoyote ambayo yanajitokeza, kuna mambo yaliyopo ndani ya uwezo wetu na mengine yapo nje ya uwezo wetu.
Sisi sio viranja wa dunia. Kufanya kazi ipo ndani ya uwezo wetu. Kazi isipokamilika ndani ya muda uliotegemea, utegemee pia hilo linaweza kutokea.
Karibu tujifunze kutoka kwa wanafalsafa wa kale walisemaje kuhusu hasira.
- Watu wanakoseshwa na ‘views’ zao, ni kwa sababu ya tafsiri zetu zinazotokea. ‘Men are not disturbed by their actions but their views on them.’
- Usiruhusu hisia zako zikuongoze, zisiwe na nguvu juu yako, angalia tukio kwa utulivu. Ukipata hasira usitoe maamuzi yote kwa pamoja, toka hapo nenda sehemu nyingine. Andika chochote kuhusu mtu huyo. Baada ya muda hasira zinaisha. Waelewe watu ili wasikupe shida.
- Ukiwa unaweza kuvumilia basi usilalalamike. Chochote kinachotokea kwenye maisha yako kinapaswa kutokea, yapokee yalivyo.
- Hakuna kinachokufanya ukasirike zaidi ya mawazo yako mwenyewe. Badilisha mawazo yako utapata amani. Mtu asipokuitikia, labda ana mawazo mengine, chukulia vitu vilivyo.
- Usiwe mtumwa wa hisia zako. Dhibiti hisia zako na akili zako zitakutii. Wenzi marafiki tumepewa kwa muda. Asili ikizitaka zitawaondoa tu mfano kifo n.k. Ukiwa mu wa hasira utaweza kufa mapema.
Rafiki hasira inaweza kutukosesha amani na utulivu kwenye maisha yetu. Tunapaswa kubadilisha mawazo yetu ili tupate amani na amani.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.