Rafiki yangu mpendwa kama wengi wananunua na wewe unakimbilia hapo kununua . Hivyo tunaamini katika wengi, wengi wanaiga kwenye kununua vitu. Wanaofanya maamuzi kwa mantiki ni asilimia 5 tu, wengine wanafuata mkumbo.
Njia kumi za kutumia kuongeza mauzo kwa kutumia social proof ni kama yafuatayo;
- Tumia wateja. Watu wanapenda waone wengine waliotumia bidhaa ndiyo watu wengine wanunue kwa mfano celebrities wakitumia bidhaa fulani inawashawishi wateja wengine kununua.
- Onyesha idadi ya wateja wanaotumia bidhaa zako. Kwa mfano vodacome ina wateja zaidi ya 15 millions . Inafanya wateja wengine kutumia mitandao hiyo.
- Matumizi ya (influencers) au wenye mamlaka. Tafuta mtu mwenye ubalozi kwenye kutangaza biashara yako. Mfano pepsi na diamond.
- Tumia ( user generated content). Wasanii wanaopenda kupata huduma.
- Endorsement from big brands kwa mfano NBC bank inavyoshirikiana na vilabu vya Tanzania.
- Matumizi ya takwimu na utafiti za masoko . Takwimu zinaongeza imani ya wateja bidhaa au huduma. Kwa mfano benki ikisema 90% ya wafanyabiashara wanatuamini kwa mikopo nafuu.
- Matumizi ya kuweka uharaka na uhaba. Watu wanapenda vitu kabla havijaisha. Mfano usiseme mzigo uko vya kutosha. Watu hawaharakishi kuja kununua.
- Maoni ya ukadiriaji wa wateja. (Ratings and reviews). Mfano app zina nyota ngapi, reviews za wateja kwa mfano booking.com, wahimize wateja waache maoni. Google reviews.
- Matumizi ya teknolojia, chat box. Maswali yanayoulizwa mara kwa mara, inasaidia wateja waone wanajibiwa haraka.
- Kuonesha miradi ya kijamii jinsi inavyofanya kazi. Kwa mfano coca-cola company kujenga visima vijijini. Inaongeza imani kwa wateja. Taasisi zinatoa pole kwa majanga, kwa mfano kariokoo jengo liliporomoka unatuma salamu za pole na kuitambulisha biashara yako. Watu wanaona unajali jamii.
Chukua hatua, rafiki wengi wanapofanya jambo fulani tunafikiri ndiyo jambo jema, hivyo hufanya wengi zaidi kufanya jambo hiyo hiyo. Kwa sababu penye wengi hapaharibiki kitu, kwa sababu wengi wape, tunapaswa kutumia mbinu hizi kwenye kutangaza biashara zetu.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.