Rafiki karibu sana leo tunajifunza kuhusu njia za kusaidia kuunda mfumo wa mauzo.
Njia hizo ni kama yafuatayo;
- Weka mfumo wa mauzo ulio wazi, ( mauzo ya uhakika bila kutegemea bahati). Mchakato unaoeleweka wa kupata wateja.
- Gawa majukumu ya mauzo. Kila mmoja kazi yake inakuwa ni kutekeleza majukumu yaliyopo kwenye biashara.
- Usitumie muda mwingi na watu wasio na nia ya kununua. Njia ya maswali ni rahisi kukufanya uweze kibaini hili.
- Uza kwa njia ya kujenga mahusiano na siyo kulazimisha. Tuwafanye wateja kuwa rafiki zetu.
- Wekeza kwenye utafutaji wa wateja kila siku.
- Tumia simu na ujumbe wa moja kwa moja kwa ufanisi.
- Tengeneza mfumo wa rufaa au (refferal) .
- Wekeza katika kuwaelimisha wateja wako.
- Andika ujumbe wa mauzo wenye ushawishi mkubwa.
- Fuata mfumo wa kujenga uaminifu kwanza, kisha uza.
- Hakikisha una data sahihi ya wateja kama jina, namba kwa usahihi.
- Kuwa na mfumo wa kufuatilia wateja mara kwa mara hadi waoneshe nia ya kununua .
- Usiogope kutafuta wateja wapya ( cold calling) unaanza kwa kwa ujumbe mdogo mdogo baadae unampigia.
- Toa huduma bora wauzie kitu ambacho ni bora.
- Usitumie bei kama sababu pekee ya kumshinda mteja. Onyesha thamani ya bidhaa yako kwanza, ili usimpoteze baada ya manunuzi ya mwanzo tu.
- Wekeza katika mafunzo. Mafunzo ya ndani.
- Tumia mitandao ya kijamii vyema.
- Tumja shuhuda halisi za wateja wenye mafanikio. Wateja wengi wanapenda kufuata mkumbo.
- Tumia mfumo wa kurahisisha malipo, ili usipoteze wateja.
- Tumia mfumo wa mrejesho wa huduma ( feedback).
Chukua hatua rafiki, wewe kama muuzaji uza kila siku, fuatilia wateja wako.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com