Jinsi Ya Kuvunja Kuanzia Sifuri.

Rafiki yangu mpendwa ukiona mafanikio ya watu wengine ujue kuwa wamepambana hadi wakapata mafanikio hayo.

Hapa kuna baadhi ya mambo ya kufanya ili kuepuka kuanzia sifuri kila mara.

  1. Badilisha mtazamo kuhusiana na fedha. Akili zetu iwaze mbali na kwa upana zaidi. Mafanikio ya kifedha ni kitu ambacho kinajengwa. Lazima tuijenge kwa watoto wetu kwa kufanya na kujenga utajiri kwa sababu watoto wanaiga yale wazazi wanafanya.
  2. Kuanza kuweka akiba na uwekezaji. Kuwafundisha watoto kuwa na tabia ya kuweka akiba na uwekezaji mapema.
  3. Kuondoka kwenye madeni mabaya. Madeni mabaya ni muhimu kuondokana nayo, madeni yanarudisha nyumba. Lazima kuwe na sababu ya kukufanya wewe ukope.
  4. Tengeneza mtandao wa watu sahihi. Mafanikio yanatokana na kukaa na watu sahihi kushirikiana nao wanatusaidia kufungua bongo zetu.
  5. Kutambua vipaji ulivyonavyo. Tutambue na kuvitumia vipaji vyetu na tuvinoe. Vipaji vya watoto wetu tuvipalilie na kuweka nguvu kwenye vipaji hivyo ili wakavitumie kuweza kusimama.
  6. Kutengeneza biashara ambayo haikutegemei wewe na inajiendesha yenyewe na watoto wanaikuta na wanamiliki kwa kufuata mfumo huo huo.

Chukua hatua; rafiki yangu vikiwemo maoni, mfumo na mauzo utakuwa umeewaacha watoto maeneo salama wataweza kuendesha maisha yao salama. Na pia utakuwa umeewaacha alama nzuri duniani.

Rafiki yako,

Maureen Kemei.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *