Katika Kuukabili Ugumu Wa Maisha, Falsafa Ya Ustoa Inasisitiza Mambo 6 Yafuatayo:

Rafiki yangu mpendwa falsafa ya ustoa ni mtazamo wa kifikra unaohimiza uvumilivu, nidhamu ya kihisia, na kuukabili ukweli wa maisha kwa utulivu.

Mambo hayo 6 ya kuzingatia katika kuukabili ugumu wa maisha ni kama;

  1. Kubali kile usichoweza kudhibiti. Maisha yana changamoto ambayo haziwezi kuepukika, kama vile magonjwa, kupoteza wapendwa au kushindwa katika mambo fulani. Badala ya kulalamika , Ustoa unahimiza mtu azikubali hali hizo kwa utulivu na aelekeze juhudi zake katika kile anachoweza kudhibiti, kama vile mtazamo wake na matendo yake.
  2. Zingatia matendo yako, si matokeo. Tunapaswa kuweka juhudi katika kufanya jambo kwa uadilifu bila kuwa na wasiwasi juu ya matokeo, kwani hatuwezi kuyadhibiti kikamilifu.
  3. Tumia changamoto kama fursa ya kujifunza. Badala ya kuona matatizo kama vikwazo, Ustoa unahimiza kuona ugumu wa maisha kama nafasi ya kukua kiakili na kihisia.
  4. Fanya mazoezi ya kujizuia ( self discipline). Ustoa unasisitiza mazoea ya kujifunza kustahimili hali ngumu kwa hiari, kama vile kujizoeza kuishi na rasilimali chache ili kuimarisha uimara wa kiakili na kuepuka utegemezi wa starehe kupita kiasi.
  5. Jifunze kuwa na mtazamo wa busara ( virtue first). Maisha mazuri kwa mujibu wa ustoa yanategemea kuishi kwa maadili mazuri kama vile hekima, ujasiri, haki na kiasi.
  6. Fahamu kuwa kila kitu ni cha muda. Maumivu,raha, mafanikio,na matatizo yote ni ya kupita. Kutambua hili kunasaidia kuwa na utulivu wa nafsi bila kushikilia sana hali fulani.

Chukua hatua; falsafa ya Ustoa inahimiza mtu kuwa na uvumilivu, nidhamu, na mtazamo chanya mbele ya ugumu wa maisha, kwa kutambua kwamba hatudhibiti kila kitu isipokuwa mawazo na matendo yetu.

Rafiki yako

Maureen Kemei.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *