Njia 5 Za Kukuwezesha Kuwa Wewe Kwenye Jamii Ya Kisasa.

Kuwa wewe mwenyewe katika jamii ya kisasa kunahitaji uwiano kati ya kujielewa, kukubali mabadiliko, na kushikilia misingi yako.

Hapa kuna njia tano za kufanikisha hilo;

  1. Kujitambua na kujiamini. Fahamu thamani zako, malengo yako na kile unachokipenda. Usiogope kuwa tofauti kwani ndiyo kunakokufanya kuwa wa kipekee. Jifunze kujikubali na kuepuka kulinganisha maisha yako na ya wengine.
  2. Endelea kujifunza na kukua. Dunia inabadilika haraka, hivyo endelea kusoma, kusikiliza na kujifunza. Jifunze kuhusu teknolojia,utamaduni, na mienendo bila kupoteza utu wako. Chagua habari na mitazamo inayokuza maarifa yako badala ya kuathiri vibaya mtazamo wako.
  3. Dumisha mahusiano na uhalisia. Kuwa na mazungumzo ya kweli na maana na marafiki,familia na jamii. Tumia mitandao ya kijamii kwa hekima, usiruhusu maisha ya mtandaoni yakufanye upoteze uhalisia wako. Dumisha maadili yako hata kama dunia inabadilika.
  4. Kubali mabadiliko lakini chuja mengine. Sio kila kitu cha kisasa kinafaa kwako; chagua kile kinachoendanaa na thamani yako. Jifunze kubadilika bila kupoteza msingi wa utu wako. Usiogope kusema ‘hapana’ kwa shinikizo la jamii ikiwa haliendani na wewe.
  5. Tumia teknolojia kwa manufaa yako. Badala ya kuwa mtumwa wa teknolojia, itumie kukuza elimu, biashara, na ubunifu wako. Dumisha uwiano mzuri kati ya muda wa mtandaoni na maisha halisi.

Chukua hatua; kuwa wewe kwenye jamii ya kisasa unahitajika kuchangamka, lakini pia kubaki na msingi wako.

Rafiki yako,

Maureen Kemei.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *