Mambo 10 Muhimu Kuhusu Kazi.

Rafiki yangu mpendwa kazi ni asili ya wanadamu. Siyo adhabu, kazi ni zawadi toka kwa Mungu, mtu asiyetaka kufanya kazi na asile chakula.

Kazi bora zaidi kuliko zingine ni ile ambayo unaifanya. Fikra na mtazamo wako ndiyo kazi bora unayoifanya.

Mambo kumi kuhusu kazi ni kama yafuatayo;

  1. Ipende kazi. Kazi yoyote unayoifanya ipende. Ifanye kwa hamasa na utapata mafanikio. Kazi ukiipenda nayo itakupenda. Ukiipenda itakua bora sana.
  2. Kuwa wa kwanza kufika na wa mwisho kuondoka. Kufanya hivyo itakutofautisha na wengine.
  3. Unapofanya kazi fanya kazi usihangaike na mambo mengine. Heshimu kazi yako na kuipenda.
  4. Fanya kazi mbili ya muda ambao wengine wanafanya kazi. Utapata matokeo mara mbili ya wengine . Rafiki pekee anayeweza kukupa msaada mkubwa ni kazi.
  5. Wanaokuambia unafanya kazi sana, jua hao hawafanyi kazi. Hao wanaokuambia huwa unafanya kazi sana wana wivu ila hawawezi kufanya kama wewe.
  6. Usiseme sio jukumu langu au siwezi kufanya. Ukipewa jukumu iwe unaweza au hujui kufanya pokea na jifunze namna ya kufanya na fanya.
  7. Kila siku ni siku ya kazi. Kama jua linachomoza basi ujue ni siku ya kazi kwako. Kila siku amka na hamasa ya kazi. Hakuna siku huli chakula.
  8. Usilalamike kuwa una kazi nyingi. Kuna wengine hawana kazi kabisa na hawajui wafanye nini. Shukuru na usilalamike.
  9. Usijidanganye kwamba unamfanyia mtu kazi. Kama ukifanya kazi bora utajijengea thamani kubwa sana. Mtu wa kwanza unayemfanyia kazi ni wewe mwenyewe.
  10. Kufia kazini ni ushujaa. Ondokana na mawazo ya kukimbia kazi bali weka kazi na jenga urafiki na kazi.

Chukua hatua rafiki yangu tunapaswa kupenda kufanya kazi kwa sababu kazi inatutambulisha kwa watu. Tukifanya kazi kwa bidii tutaheshimika zaidi.

Rafiki yako,

Maureen Kemei .

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *