Rafiki yangu wanasema ni kwenye muda pekee ndipo penye demokrasia ya kweli duniani. Ndiyo kitu pekee ambacho tumepewa kwa usawa.
Kwa kuwa tumepewa kwa usawa, ila wapo ambao wanafanya makubwa sana kwenye muda huo huo, ina maana kuna vitu wanafanya kwa utofauti.
Dr Kocha Makitita Amani anasema kuwa siri kuu ya kutumia muda vizuri ni kusema hapana kwenye mambo yote ambayo hayana mchango kwenye maisha yako na mafanikio unayotaka.
Mambo hayo ni kama yafuatayo ;
- Kufuatilia habari kwa tv, redio magazeti na vyombo vingine vya habari.
- Matumizi ya mitandao ya kijamii, hii inaleta urahibu wa kuzurura na hamu ya kutaka kujua ni nini jipya kimetokea, watu wengi kwa kufanya hivyo wanajipata wakipoteza muda wao mwingi bila kufanya chochote cha maana.
- Ushabiki wa michezo wa aina yoyote ile, Kocha anasema kwa kuwa mrahibu wa kufuatilia michezo mbalimbali unajipata umepoteza muda wako mwingi.
- Vikao visivyo vya lazima vya jamii na familia. Ukiwa mtu wa kufuatilia na kuhudhuria vikao mbalimbali kwenye jamii hutakuwa na muda wa kutosha wa kufanya shughuli zako za maendeleo.
- Ulevi na starehe mbalimbali . Ukiwa mtu unayependa starehe za anasa na pia kuzungukwa na marafiki wanaopenda starehe kama hizo utajipata hutaweza kufanya makubwa kwenye maisha yako.
Chukua hatua; rafiki kwa kusema hapana kwenye hayo, unabaki na muda mwingi ambao unaweza kuutumia kwenye mambo yenye tija zaidi.
Tunapaswa kuilinda sana muda wetu, kwa kutumia neno hapana kwa yote yasiyokuwa na mchango kwenye mafanikio unayoyataka.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.